Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi. Tukichukulia kunywa maji ya kutosha ni mithili biashara kati ya wewe na afya yako, biashara hii inalipa. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha .
1.Kusaidia mmeng’enyo wa chakula.
Vimengenya na Kemikali mbalimbali zinazohusika na mmen’genyo au usagaji wa chakula mwilini ziko katika hali ya mchanganyiko na maji. Ili hivi viweze kufanya kazi vizuri inatakiwa kuwe na uwiano sahihi kati yake na maji.Pia maji yanahusika katika kulainisha baadhi ya vyakula. Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.
2.Dawa ya maumivu ya kichwa.
Mara nyingine maumivu ya kichwa yanasababishwa na upungufu wa maji mwilini. Hii inamaanisha, kama una maumivu ya kichwa yanayosababishwa na upungufu wa maji mwilini unaweza kughairi kumeza vidonge vya
kutuliza maumivu na kunywa maji. Hii inawezekana kwenye baadhi ya maumivu ya mgongo pia.

3.Kuboresha afya ya ngozi. 
Pendezesha ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha, Unaweza kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha kwani maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza unyevu kwenye ngozi .
4.Kusaidia akili yako.
Maji yanauweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi zaidi. Kunywa maji ya kutosha kunamwezesha mtu kufikiria kwa ufanisi zaidi.
5.Kutatua tatizo la kukaukiwa haja kubwa (constipation)
Sehemu kikubwa ya haja kubwa ni maji. Kunywa maji ya kutosha kunaweza kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara kwa nyingi zaidi.
6.Kuboresha hali ya viungo na misuli
Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.
7.Kuondoa uchovu
Maji yanachochea shughuli za kimetaboliki mwilini na kuongeza ufanisi wa ubongo kwa hiyo yanapunguza uchovu.
8.Kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa.
Uwezekano wa kupata mafua,mawe ya figo,matatizo ya ini,baadhi ya saratani n.k, unaweza kupunguzwa kwa kunywa maji ya kutosha .
9.Maji yanaweza kusaidia katika kupunguza uzito.
Kama uko katika mkakati wa kupunguza uzito maji yanaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa. Maji huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki mwilini. Ongezeko hilo la kimetaboliki husababisha mwili kutumia nishati nyingi zaidi na hivyo huweza kupunguza kiasi cha nishati ambacho kitahifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta au kupunguza kiasi cha nishati kilichohifadhiwa mwilini.Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini kutokana na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya ziada mwilini.
Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.
“Usinisingizie.Sijasema ushindie maji asubuhi mpaka jioni.”

10.Maji ni kiburudisho
Kunywa maji ya kutosha kutakufanya ujisikie vizuri na pia kunaweza kupunguza safari za hospitali. Kunywa maji ya kutosha, fanya siku yako iwe poa zaidi. Zingatia sana matumizi ya maji hasa kwa wakati huu wa joto kali ili kuepukana na matatizo yasiyo ya lazima.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv


 
Top