Melanie
Trump ambaye ni mke halali Rais mteule wa Marekani Donald Trump, alizaliwa
April 26,1970 mjini Novo Mesto Yugoslavia. Alizaliwa na kupewa jina la Melanija Knavs baadae akabadilisha kuwa Melania Knauss.
Baba yake
alikuwa anajishughulisha na biashara ya magari huku mama yake akiwa
mwanamitindo na mtengenezaji wa nguo za watoto. Aliishi kwenye familia ya
kawaida akiwa na mdogo wake wa kike mpaka baadae alipogundua kuwa na kaka
mkubwa ambaye baba yake alimpata kwenye mahusiano kabla ya kuwa na mama yake.
TUANZIE KATIKA UREMBO & ELIMU
Alipofikisha
maika 16 akaanza kujihusisha na mambo ya fashion na mitindo, baada ya miaka
miwili akasajiliwa kwenye moja ya mashirika yanayojihusisha na mitindo huko
Milan. Japokuwa alikuwa akiendelea na masomo katika chuo cha Ljubljana, aliacha
shule ili aweze kuendeleza kipaji chake, ingawa Tangu mwaka 2006 Melanie
amekuwa akisema alishamaliza Degree yake ya masomo ya Uhandisi chuoni hapo
Mwanzoni
alikuwa akifanya kazi mjini Milan na Paris kabla ya kuhamia New York mwaka 1996
ambapo ndipo alipopata makazi ya kudumu kikazi na aliweza kufanya kazi na
wapiga picha maarufu kama Patrick Demarchelier na Helmut Newton huku akitokea
kwenye kurasa za mbele za majarida makubwa ya fashion.
HADI KUKUTANA DONALD TRUMP MPAKA NDOA
Mwaka
1998 Melania alikutana na Donald Trump huko New York katika party ya fashion,
japokuwa mwanzoni alimtolea nje Trump, baadae wakaelewana na kuanza kuweka
mahusiano yao hadharani na mwaka 2004 Trump akamvisha pete ya uchumba. Mwaka
uliofuata 2005 wakafunga ndoa huko Palm beach Florida, sherehe ambayo
ilihudhuriwa na mastaa wakubwa, pamoja na Rais Bill Clinton na mkewe Hillary
Clinton ambaye wakati huo alikuwa seneta kwenye jimbo la New York.
Mwaka 2006
Melania alijifungua mtoto wa kwanza, Barron William Trump ambaye kwa Trump yeye
ni mtoto wa tano. Mwaka huo huo Melania akawa raia rasmi wa Marekani.
WAKATI WA KAMPENI ZA URAIS
Wakati
Donald Trump alipotangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi 2016, kama
ilivyokuwa kwa Michelle Obama, Melanie alianza kujihusisha na jamii huku
akipokea maoni mabaya yaliyokuwa yakihusisha picha za utupu alizowahi kupiga
wakati akiwa model mwaka 2000 huku raia wakilalamika kuwa sio mfano wa kuigwa kwa
jamii kutokana na picha zake nyingi za utupu zilizosambaa mitandaoni.
Maneno
hayakuishia hapo, July 2016 Melania alitoa hotuba makao makuu ya chama cha
Republican ambayo maelezo mengi yalifanana na yale ya Michelle Obama wakati
alipokuwa akitoa hotuba yake 2008 makao makuu ya chama cha Democratic Marekani
ambapo iliibua mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari.
Baadae mwandishi wa Trump
Meredith McIver, akakiri kukosea na yeye ndiye alichanganya kwa bahati mbaya
ripoti ya Melanie na baadhi ya maneno yaliyokuwepo kwenye hotuba ya Michelle.
Mwezi huo huo july 30,2016 gazeti la Ney York Post likachapisha picha za utupu
za Melania Trump akiwa na miaka 25, ambapo alionekana akiwa na mwanamke
mwenzake, picha ambayo baadae ilifutwa.
Baada ya sekeseke hilo Trump
aliwajibu The New York Post kuwa Melania ni moja kati ya models wenye mafanikio
makubwa na amepiga picha nyingi kwenye covers za majarida makubwa na picha hiyo
ilichapishwa kwenye jarida la Uingereza na ndilo lilimuwezesha kumfahamu
Melania.
November
2016, Melanie alitoa hotuba fupi wakati wa kampeni na akieleza ni kitu gani
atakachofanya ili kuzuia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kama atakuwa
first lady wa Marekani na kusema kuwa ‘Tunapaswa
tunapaswa tuwafundishe vijana wetu maadili ya kimarekani, wema, uaminifu,
heshim, huruma, upendo, maelewano na ushirikiano’
Melania
ana duka kubwa maarufu la vito vya thamani pamoja na bidhaa za ngozi.
Aidha
ameshawahi kutangaza kipindi maarufu cha The View pamoja na kuonekana katika Reality Tv
Show ya mumewe inayoitwa Celebrity Apprentice.
Kingine
kutoka kwa Mke wa Rais Mteule Melania Trump ni kwamba na uwezo wa kuongea
vizuri lugha tano ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kislovenia
na Kiserbia
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv