Hili ni tatizo linawakuta walio wengi sana hasa wanawake karibu
sasa hii iko hivi. Hali hii hutokana na viungo vya uzalishaji wa vichocheo
vya uimarishaji uzazi kwa mwanamke na mwanaume kutofanya kazi. Viungo
au Glandi hizi ni korodani kwa mwanaume na ovari kwa mwanamke.
Tatizo hili linaweza kuwa linatokea tangu kuzaliwa au linatokea
katika mfumo mzima wa mwili. Kwa tatizo la kuzaliwa nalo, korodani au
vifuko vya mayai huwa havifanyi kazi ya kuzalisha vichocheo au
homoni zinazohitajika ambapo kwa korodani huzalisha homoni za kiume na ovari huzalisha
homoni za kike.
Vyanzo vya matatizo
ni kama vile:-
– Matatizo katika mfumo wa kinga mwilini.
– Matatizo katika mfumo wa vinasaba.
– Matatizo ya ini na figo.
DALILI ZA TATIZO
Dalili kwa mtoto wa kike ambaye hajavunja ungo, utamwona bado ni
mtoto yaani habadiliki yupo vilevile tangu alipokuwa na umri wa miaka
kumi hadi anafikisha ishirini, matiti hayakui, urefu haongezeki.
Kama tatizo likitokea baada ya kuvunja ungo huhisi joto muda wote hata
kama kuna baridi, nywele sehemu za siri na makwapani hupuputika
zenyewe, hupoteza hamu ya tendo la ndoa kabisa na haendelei tena kupata
siku zake na kufunga hata zaidi ya mwaka.
Ukiwa na dalili
hizo, muone daktari kwa ushauri zaidi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv