Kwa walio wengi sasa
hasa madada wanapenda sana kupiga selfi yaani picha za kujipiga mwenyewe kwa
baadhi ya madada selfie ndio kila kitu utafikiri walisoma
photojournalism; yani kila mara popote alipo ni kujitwanga picha na hivi siku
hizi kuna powerbank ndio kabisaa hawahofii kwamba simu itazima.
Sasa taarifa ikufikie
wewe mpenda picha za selfie kwamba takwimu za utafiti uliofanyika hivi karibuni
juu ya vifo vinavyochangiwa na upigaji picha vimekuwa vikiongezeka kila uchwao
kwani mwaka 2014 walikufa watu 15, 2015 wakafariki watu 39 na mwaka huu kwa
kipindi cha miezi nane ya awali tayari wamefariki watu 73.
Utafiti uliofanywa na
Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Hemank Lambawa akishirikiana na wenzie wa
Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon huko Pittsburgh umegundua njia ya
kukabiliana na vifo hivyo ni kutengeneza App maalumu itakayokuwa ikitoa
ishara mara mtumiaji awapo kwenye hatari ili aweze kujihami.
Tazama baadhi ya picha
ambazo watu wamekuwa wakipiga selfie licha ya kuwa kwenye hatari ya kupoteza
maisha.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv