Karibu sana msomaji wa edonetz  katika mfurulizo wa makala ninazokuandalia kila siku nakwa siku ya leo bhasi sio vibaya tukiasgazia hili kiundani zaidi ,tukiongelea Uchovu wa mara kwa mara na kuchoka, huweza kusababishwa na zaidi ya usingizi. Au unafikiri upo ulivyo kwa sababu nyingine?
Kutopata usingizi wa kutosha ni moja ya sababu inayoweza changia uchovu, ila uchovu wa mara kwa mara na kujiona umetumika  ilhali umepata usingizi wa kutosha inakera. , hii imekuwa ni hali ya kawaida kwa wengi wetu , ila sio hali ya kawaida, na kwsababu kadhaa au pengine za kihisia.

Matibabu
 Kupuuzia maumivu au dalili za maradhi  ni kitu kibaya, kwani yaweza kuwa ni dalili ya ugonjwa, upungufu wa damu au tezi, yaweza kuwa tatizo la kawaida , ila uchovu ni moja ya dalili ya baadhi ya magojwa mengine, kama kisukari. kama umekuwa ukijsikia uchovu kwa zaidi ya wiki mbili, nenda kamuone daktari kwa ajili ya chekap, kama hamna la zaidi tuliza mwili na akili yako

Mpangilio wa chakula
Chakula ni mafuta ya miili yetu kwa hiyo kama hatupati chakula cha kutosha, nguvu ya miili yetu hupungua, ila inaweza sababishwa na kitu chocote,  yaweza kuwa diet ya kupitiliza, au kula vyakula ambavyo havitukubali., ila umeshindwa kuvishtukia, kama unataka kupunguza uzito, hakiksha unafanya hivyo kwa taratibu, kiafya , weak kumbukumbu ya chakula unavyokula ambayo utamuonesha daktari wako, hii yaweza saidia kutambua kama kuna vyakula vinavyo kudhuru.

Uzito wako
Kama una uzito mkubwa, hii yaweza changia uchovu wa  mara kwa mara, kwa sababu mwili wako, utahitaji kutumia nguvu ya ziada, kuuhimili.hupelekea uzito wa ziada kwenye viungo vyako, moyo na mapafu, na kuwa na uzito mkubwa napo huumanisha misuli yako inakazi ya ziada

Mashaka na msongo wa mawazo
Usingizi unachangiwa kwa kiasi kikubwa na afya ya aklii, mashaka, na mishipa ya fahamu yaweza changia kukosa usingizi insomnia, kitu ambacho baada ya muda, yaweza kuwa sugu na kukuwacha mwenye kudhoofika. kama una msongo wa mawazo kujikuta ni mwenye kulala kila waakati,  napo ukaendelea kuwa  mwenye uchovu  mwenye kuw a hali hii ikijitokeza kwa muda mrefu basi ni busara kuomba msaada
Tungi
Pombe yaweza saidia kupata usingizi, ila ni mbaya kutumia kama chanzo cha kupatia  usingizi, haitatui mzizi wa chanzao wa tatizo lenyewe., vile vile pombe za kupitiliza  yaweza kupelekea kushtuka katikati ya usiku wa manane, na hatimaye kuwa na usingizi wa mashaka na watabu, kwa hiyo kunywa mara tu kabla ya kulala ni mbaya kiafya

Maji
Ni Moja ya sababu inayowapeleka wanawake wengi kujikuta wakipigana na uchovu. jaribu kunywa maji megni unapoamka, japo glasi mbili kila unapopata msosi, yaweza kuleta utofauti, pata chai na juice katika kila hatua ya siku yako, hii itakuongezea kiwango cha nguvu zako
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv


 
Top