Walio wengi wanapenda kuingia kwenye mapenzi tu washiriki tendo hila hii haikuzi pendo na kama hautakuwa makini basi unaweza kukuta mapenzi yanakufa kabisa kwa sababu hamjasomana vya kutosha so ni vizuri sana kusomana kabla ya kushiriki tendo , na kuna baadhi yaw engine hawataki kushiriki hila wanashindwa kujizua .hila leo jifunze jinsi gani unaweza kujizuia kiujumla usisahau  #kutufollow
1.    Usilale kwake

Iwapo hautaki kufanya mapenzi na mpenzi wako, basi ni vizuri usijiingize katika hali ambazo zitachangia nyinyi wawili kuingiwa na hamu ya mapenzi. Iwapo umetoka deti na mpenzi wako, usijaribu kumsindikiza hadi kwake ama kuenda njia moja. Pia hutakiwi kuwa unazunguka sehemu ambazo mpenzi wako anaishi wakati kama huo kwa sababu inaweza kuchangia pakubwa kuingiwa na tama

2. Usiwe mlevi

Kuna baadhi ya watu wanafikiria ya kuwa matumizi ya vinywaji ukiwa na mpenzi wako inapunguza hisia za kufanya mapenzi. Well, labda inaweza kuwa ni kweli lakini kulingana na utafiti ni kuwa mtu mlevi anapoteza mwelekeo wa kufanya maamuzi yafaayo. Hivyo ukiwa umeathirika na ulevi pamoja na mpenzi wako, kuna asilimia kubwa ya kufanya maamuzi ambayo si sawa.

3. Toa visababu ambavyo havitomkwanza mpenzi wako

Unaweza kutoa visababu kama vile unaumwa na kichwa, hujiskii vizuri nk. Ingawa kutumia uongo kwa mpenzi wako si jambo zuri, ni muhimu sana iwapo itakuja kwa maswala ya kufanya mapenzi ama kama hujiskii kufanya mambo mengine ambayo yanahusiana na wewe. Hivyo ni muhimu kupatia mambo mengine kipao mbele.

4. Fungua roho yako

Hii ndio njia nzuri zaidi kujizuia kutofanya mapenzi. Kukaa na mpenzi wako katika kikao na kumueleza ndani na nje kuhusiana na wewe kujizuia kutofanya mapenzi ni jambo nzuri zaidi kwa nyote wawili. Kumueleza ukweli mpenzi wako kutatoa ile nafasi ya kwako kuonekana kama unayapenda mahusiano yenu na hauhitaji kuficha ama kudanganya katika mahusiano yenu.
Iwapo atakubali basi itadhihirisha ya kuwa yeye anatilia maanani mahusiano yenu. Kama atakataa basi bila shaka mahusiano yenu hayatokuwa marefu.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top