Karibu sana mtu mtu mkubwa tuangazie hili kiundani zaidi Tunapozungumzia
mwanamke kukosa uwezo wa tendo la kujamiiana hapa tunamaanisha anakuwa
hana hamu ya tendo hilo au hata akilifanya hafurahii.
Uwezo wa kufanya tendo la kujamiiana kwa mwanamke
tunategemea unapungua taratibu kuanzia umri wa miaka hamsini, siyo unaisha
ila unaanza kupungua taratibu kadiri umri unavyosonga mbele hadi
baadaye unaisha kabisa.
Katika umri huo ndipo tunategemea kusikia mwanamke anaanza
kusema hamu ya tendo hilo inapungua au imepungua na hata akilifanya
hafurahii kama zamani, hii inatokana na upungufu wa vichocheo muhimu vya ‘Estrogen’ ambavyo ni lazima
vipungue katika umri huo ambao mwanamke tayari ameshafikia ukomo wa hedhi
na uzazi. Endapo vichocheo hivi vitaendelea kuwa juu katika umri huo au
ataviongeza, basi kuna hatari ya mwanamke kupata saratani ya mfuko wa
uzazi.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Hali ya kutohisi hamu ya tendo na kutopata raha ya tendo ni ya
kawaida katika umri mkubwa wa mwanamke kuanzia miaka 50 lakini si ya
kawaida katika umri wa chini ya hapo, siyo kawaida kwa mwanamke wa umri
wa miaka 20 hadi 48 kupata tatizo hili. Endapo mwanamke wa umri
huu atalalamika hali hiyo basi ni tatizo linalohitaji uchunguzi wa kina.
Katika umri wa kuzaa, pale mwanamke anapoendelea kupata siku
zake kama kawaida tunategemea mwili wake upo vizuri, homoni zake zinafanya
kazi vizuri na anafurahia maisha yake.
Kutohisi hamu ya tendo la ndoa ni kutopata hisia za kimapenzi
hata akimuona mwenzi wake, akiguswa au hata akiambiwa maneno ya
mapenzi hapati hisia wala msisimko wowote wa kimapenzi. Mwanamke
asiyefurahia tendo la ndoa ni yule asiyefikia kilele cha tendo hilo,
mwanamke akifikia kilele hutoa majimaji na huwa na hali ya kumaliza tendo na
kupumzika lakini akiwa na tatizo hili hafikii hapo na hufanya tendo hilo
basi tu na humridhisha tu mpenzi wake.
DALILI ZA TATIZO
Mwanamke mwenye tatizo la kutohisi hamu huwa yupo tu na anaweza
kukaa muda mrefu hata zaidi ya mwaka bila kufanya tendo hili na hana
tatizo lolote, huendelea tu na shughuli zake. Mwenyewe atakuambia
labda mwenzake amuanze lakini vinginevyo hajisikii hamu kabisa.
Kitaalamu hawezi kupata tatizo lolote kiafya labda kama yupo kwenye
uhusiano ndiyo italeta mgogoro. Mwanamke asiyefurahia tendo anaweza
kuwa na historia ya kuwa na maumivu wakati wa tendo, kama alishawahi
kuingiliwa kwa nguvu au kama mwenzake yaani mume ana matatizo wakati wa
tendo aidha hawezi au hamfikishi mara kwa mara.
Kutofurahia tendo kwa muda mrefu humuathiri mwanamke katika afya
yake ya akili na hulifanya kwa kujilazimisha. Wanawake wengi wenye
tatizo hili chanzo huwa ni wanaume kushindwa kumudu tendo hili.
MATIBABU NA USHAURI
Tatizo hili halina dawa maalumu, jambo la msingi ni kujua chanzo
chake na kukitibu. Uchunguzi utazingatia mambo mbalimbali kutegemea
na daktari atakavyoona inafaa.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv