Tukiongelea
Kupata mlo kamili ni huhakikisha mama anapata virutubisho vyote muhimu na
kwenye kiwango sahihi kwa mahitaji yake na mtoto anayekua. Njia rahisi ya
kuapta mlo sahihi ni kupata kiwango kinachotakiwa cha chakula kutoka katika
kila kundi la vyakula. Umuhimu wa lishe bora ni kuufanya mwili kuongezeka
uzito, kuzuia upungufu wa damu, kuboresha ukuaji na maendeleo ya mtoto aliyepo
tumboni. Mlo kamili hutokana na vyakula mchanganyiko kutoka kwenye makundi yote
muhimu ya vyakula. Kwenye makala yetu ya leo tunaangalia vyakula muhimu kwenye
kujenga afya ya mama na mtoto anayekua tumboni.
Yafuatayo
ni makundi tofauti ya virutubisho vya chakula yanayotakiwa kupewa kipaumbele
kwenye mlo wa mama mjamzito.
Wanga
ni chanzo kikubwa cha nguvu mwilini. Vyakula vya wanga vimegawanyika katika
makundi matatu wanga, sukari na ufumwele. Vyakula hivi hupatikana kwa wingi na
kwa urahisi zaidi kwenye nafaka kama mahindi,mchele, mtama, ulezi na ngano.
Vilevile, vyakula hivi hupatikana kwenye vyakula vya mizizi kama mihogo, viazi
vikuu, magimbi na viazi vitamu. Vyakula hivi huusaidia mwili wa mama
kutengeneza mafuta, kuupa mwili joto na nguvu. Ukosefu wa vyakula hivi
huusababisha mwili kukosa mafuta, kudhoofika kwa nyama za mwili na kupungua
uzito.
Vyakula
vinavyotokana na wanyama kama mayai au maziwa vina virutubisho muhimu sana kwa
mama mjamzito. Mama anapata vitamin, madini na virutubisho vingi sana kutoka
kwenye maziwa. Kwenye maziwa yanapata madini ya Calcium ambayo husaidia ukuaji
wa mifupa ya mtoto.
Vilevile
kuna protini, vitamin D na phosphorus. Ieleweke kuwa mama mjamzito anahitaji
protini asilimia 60 zaidi ya kiwango anachohitaji mama asiye mjamzito.
Vyakula
hivi ni vyanzo vya protini, ufumwele na vitamin kwa wingi. Ni vyakula ambavyo
havigharimu fedha nyingi na vinapatikana kwa wingi. Maharage yana kiwango
kikubwa sana cha protini ambayo hutumika mwilini moja kwa moja bila kuleta
madhara zaidi mwilini.
Vyakula
vyenye mafuta ni kama vile alizeti, nazi, mawese, omega 3 na mbegu zinazotoa
mafuta. Mafuta yakiongezwa kwenye chakula huboresha usharabu wa baadhi ya
vitamin na huongeza kiasi cha nishati. Kuna baadhi ya samaki wana mafuta yenye
uwepo wa virutubisho vya omega-3 ambavyo husaidia kuboresha ubongo, hasa wa
mtoto anayekua. Virutubiosho hivi pia hupatikana kwenye mayai ya kuku wa
kienyeji. Mafuta haya humsaidia binadamu kua na uwezo mkubwa wa kufikiria na
kutunza kumbukumbu. Pia mafuta husaidia mtoto kuzuia magonjwa kama autism,
kisukari. Pia ni kinga nzuri kwa mama kwenye kuzuia kifafa cha mimba.
KUMBUKA
Mama
mjamzito anatakiwa kupata gramu 250 za mafuta kila Siku kwa kipindi cha mwisho
cha ujauzito. Hii itasaidia kujenga ubongo na mfumo wa fahamu wa mtoto.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv