karibu sana msomaji wa edonetz kwa mara nyingine tena nimekusogezea makala hii juu ya afya ya mtoto leo tugusie kukaa umri sahihi. karibu
Kukaa
kwa mtoto (sitting milestones) ni hatua ya kwanza kwa mtoto ndio nyingine
zinafata kama kutambaa,kusimama na kutembea, wazazi wengi wanasubiri hii
stage ya kukaa ili nao wapumzike kumbeba beba.
Mtoto
anapofikisha miezi 3 shingo yake inakuwa imeshakaza ingawa kuna wengine
shingo zinachelewa kukaza ukuaji wa watoto unatofautiana mzazi usije ukapanic
ukiona mtoto kachelewa.Kwenye ukuaji wa watoto ni zoezi linalochukua mda mzazi
hutakiwi kumfunza mapema mtoto kukaa au kutembea kabla ya mda wake.
Dalili za mtoto anaetaka kujifunza kukaa
Utakapo
mlazimisha mtoto kukaa kabla ya mda wake utamuumiza mgongo au hata kumtegua uti
wamgongo.Hakikisha mtoto wako misuli( muscles) zake zimekaza za
shingo (hainesi nesi ukimbeba),misuli ya tumbo,mgongo,miguu na mabega
nayo iwe imeshakaza na ukimbeba utamwona anataka kukaa mwenyewe iyo nayo ni
ishara kubwa.
Kukaa
kwa mtoto kunaanza akiwa na miezi 4-7 kuna wanaowahi kukaa au wakuchelewa kukaa
,unatakiwa umpe support akiwa anataka kukaa unaweza mwekea mto kwenye kona ya
sofa ukamkalisha lazima uwe pembeni yake ili asianguke , mkalisha chini
ukamshika mgongo wake kwanyuma kumpa support tumia dakika 5-10 kwa siku ukiwa
unamfunza kukaa.
Hakikisha anakuwa na toys za
kuchezea,ukiwa unamchezesha mwonyesha toys na itamfanya kunyoosha shingo
kuziangalia inamsaidia kukaza misuli ya shingo kipindi amekaa au amelalia tumbo
(tummy),mnunulie
toys za rangi rangi na zenye milio tofauti unaponunua hakikisha unanunua ya
kulingana na umri wake ,usimnunulie za watoto wakubwa zikamuumiza pindi
achezeapo.
Kwenye
kumfunza mtoto kukaa mzazi unakaa chini tanua miguu yako mkalishe chini
mtoto katikati ya mapaja yako kiasi cha kwamba akianguanguka ataangukia kwako
kwa usalama zaidi,kuna viti vya kumfunza mtoto kukaa vinaitwa bumbo floor seat
ila utakapo mkalisha mweke sehemu flat sakafuni hakikisha umemfunga mikanda
pindi akaliapo hiko kiti.
ushauri na mazingatio
Kuwa
makini sehemu utakayo mweka kulalia tumbo au kuajifunza kukaa isiwe kitandani
au juu ya meza,iwapo utamlaza/ mkalisha kitandani hakikisha uponae karibu
ili asianguke, na kama ni chini kuwe kusafi kusiwe na vitu vya yeye
kuokota na kuweka mdomoni.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv