Katika
elimu mpya kabisa ya uzazi ambapo
mwanamke yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kama si asili
ya ukoo wake. Tunaweza kusema mwanamke yeyote kwa sababu kuna imani ya miaka na miaka
kwamba, si kila mwanamke anaweza kupata ujauzito bali itategemea na asili yake.
Na kuna Baadhi ya mila na desturi, hasa
katika nchi za Kiafrika zinaamini kwamba, mwanamke kupata watoto mapacha
kunatokana na urithi wa kizazi chake, kuanzia mababu wa upande mmoja kati ya
wanandoa hivyo uzao huo hufuata mkondo kwa miaka na miaka. Wengi wakipata mapacha
huulizwa kama kwenye kizazi chake, kuna watoto mapacha. Akitokea mama akasema
hakuna, basi huaminika kwamba lazima upande wa mwanaume kuna waliowahi kuzaliwa
mapacha
kwa mfano: Mwanamke ambaye mke wa mjomba wake
ana mapacha haimpi yeye nafasi ya kupata mapacha kwa sababu hana uhusiano na
mke wa mjomba wake kibailojia. Ila mwanamke ambaye dada yake ana mapacha inampa
uwezekano wa kupata watoto mapacha kwasababu wana uhusiano wa moja kwa moja.
Hembu tujifunze hatua moja baada ya
nyingine. Na kisha tuone jinsi gani mimba ya watoto mapacha inavyotungwa.
Kwanza tujue Mimba inatungwaje?
Kipindi cha ovulation ndipo ambapo
mwanamke anaweza kushika mimba. Ovulation ni kipindi ambacho yai kubwa ama yai
lililo tayari hutoka kuelekea kwenye tumbo la uzazi kupitia mirija ya ovari.
Yai hilo kwa bahati nzuri likikutana na mbegu ya kiume hurutubishwa katika
kipindi cha masaa 24 (baada ya muda huo yai hupoteza uwezo wake). Iwapo yai
litarutubishwa ndani ya muda huo na kisha kujikita katika mfuko wa uzazi basi
mimba itakuwa imetungwa. Iwapo yai halikurutubishwa hutolewa nje kama damu ya
hedhi.
Na sasa tuangalie Mapacha hutokeaje?
Hapa tukumbuke kuwa kuna mapacha wa
aina mbili: Mapacha wanaofanana (Identical twins) na Mapacha wasiofanana (Fraternal twins).
Mapacha wasiofanana hutokea pale mwanamke anapotoa mayai mawili kuelekea kwenye
tumbo la uzazi. Hii ina maana ni mwanamke ama mwili wa mwanamke unaosababisha
mayai mawili kuachiliwa kwa pamoja. Baada ya hapo mayai haya hukutana na mbegu
za kiume ambapo hurutubishwa ndani ya muda maalumu na kisha hujikita kwenye
mfuko wa uzazi. Hivyo basi hata kama mwanaume angetoa mbegu milioni moja lakini
yai la mwanamke likitoka moja basi mtoto atakayepatikana atakuwa ni mmoja tu.
Huo ni upande wa mapacha wasiofanana
(Fraternal
twins). Kwa upande wa mapacha wanaofanana (Identical twins) hadithi ni tofauti
kidogo. Baada ya yai kurutubishwa na mbegu ya kiume na kujikita kwenye mfuko wa
uzazi kwa sababu zisizofahamika kisayansi huamua kujigawa na kutengeneza watoto
mapacha. Mapacha hawa kwa kawaida hufanana sana na huwa ni wa jinsia moja tofauti
na fraternal twins ambao huweza kuwa wa jinsia mbili tofauti ama jinsia moja.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu
inaonyesha kwamba watoto mapacha wanaofanana ama wasiofanana husababisha na
mwanamke ambaye kwa sababu moja ama nyingine mwili wake huachilia mayai mawili
ama hugawanya yai lake lililorutubishwa na kusababisha watoto mapacha. Japokuwa
kumekuwa na mabishano makali ambapo watu wengine wamekuwa na maoni hususani kwa
upande wa mapacha wanaofanana kwa kusema kwamba mbegu ya kiume huwa na nguvu zaidi
na hivyo kugawanya yai. Sina uhakika na jambo hilo ila kwa tafiti nyingi
zilizofanywa na wanasayansi zinasema mwanamke ndiye mwenye uwezo wa kusababisha
watoto mapacha yeye ama ndugu zake wa kike (wanaohusiana kibaiolojia).
Na hizi ni Sababu nyingine zinazoweza kuchangia
watoto mapacha
1. Mwanamke anayetoka kwenye familia
ambayo wanawake wana historia ya kupata mapacha.
2. Wanawake wenye asili ya kiafrika
na kimarekani.
3. Wanawake wanaobeba mimba wakiwa
na umri mkubwa, kuanzia miaka 35.
4. Wanawake wanene na wale warefu.
Kwa kuhitimisha
Kwa kifupi kama huna sababu
zilizotajwa haina maana kwamba hauna uwezo wa kupata watoto mapacha. Uwezekano
huo upo ila ni kwa kiwango kidogo kama wanawake wengine duniani. Kumbuka sababu
zilizotajwa hapo juu hazihusiani na mapacha wanaofanana, inavyosemekana
mwanamke yoyote ana uwezo wa kupata mapacha wanaofanana hata kama kwenye
familia yake hakuna historia hiyo.
Nb
Maelezo yote yaliyotolewa hapa
hayana maana kwamba ndiyo ukweli kwa asilimia mia moja la hasha kuna baadhi ya
watu kwenye familia zao wanaamini kwamba watoto mapacha waliowapata wametokana
na upande wa baba. Ila kwa asilimia kubwa inavyosemekana na wataalam wa masuala
ya uzazi watoto mapacha husababishwa na mama pamoja na wanawake kutoka kwenye
familia yake. Kama unataka kujifunza zaidi nakushauri soma zaidi tafiti
mbalimbali.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv