Kuna vitu unaweza
kuamini na vingine unaweza kuamini lakini kutokana na tafiti hizi tunaweza
kuamini katika ulimwengu huu. Amini usiamini panya ni kiumbe wa ajabu ambaye
wengi humhofia kutokana na tabia yake ya kung’ata na kupuliza; ni kiumbe pekee
anayeweza kukung’ata na maumivu yake ukaja kuyasikia baadae kabisa. Lakini si
hilo tu pia kiumbe huyu huogopwa kwa uchafu na hasa ugonjwa wa tauni.
Lakini tofauti na
unavyofikiri panya ni mnyama wa kupendeza kwani utafiti mpya umebaini wanapenda
sana kucheka. Watatifi kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt cha Ujerumani wamegundua
ubongo wa panya una neva inayohusiana na vitendo vya kucheka.
Watafiti Shimpei
Ishiyama na Michael Brecht wamepima shughuli za neva husika kwenye ubongo wa
panya na kutafiti mabadiliko ya shughuli hizo kabla na baada ya kuwashwa.
Utafiti unaonesha panya wakiwashwa, wanacheka sana na kucheza dansi kama
waliofurahishwa, na inaonekana kwamba hata panya wanajua mikono ya binadamu
itawawasha. Lakini vicheko vyao ni vya ‘ultrasonic’ na havisikiki na binadamu.
Kabla ya hapo wanasayansi walifikiri neva hizi zinahusiana na hisia ya kugusa
tu, lakini utafiti huo mpya unaonesha kuwa neva hizi pia zinahusiana na hisia
ya furaha.
Pia watafiti
wamejaribu kuchochea neva husika za panya badala ya kuwafanya wawashwe moja kwa
moja, majaribio yanaonesha kuwa neva hizi zikichochewa pia panya wanacheka.
Lakini panya wakiwa
katika hali ya wasiwasi kwa mfano wakiwekwa kwenye mahali pa juu sana,
kuwawasha au kuchochea neva zao hakutawachekesha. Wanasayansi wamesema jambo
hili huenda linamaanisha kuwa mmoja akicheka baada ya kuwashwa hakika ana
furaha moyoni.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv