KILA kitu uwaga kina kazi mwilini katika mfurulizo wa makala hizi
leo tuangazie ganda la chungwa ila ukizingatia itakusaidia sana fuata utaratibu
vizuri ,Watu wengi husumbuliwa na ugonjwa wa mba kichwani na mara nyingi mba
huwatokea nyakati za baridi kwani kichwa huwa ni kikavu sana; kama unasumbuliwa
na hilo tatizo unatakiwa kuwa makini na mafuta unayotumia na kuhakikisha
unatumia mafuta kila unapoosha nywele zako.
FANYA HIVI!!!
Chukua chungwa limenye upate maganda yake baada ya hapo chukua
limao likamue kisha uweke kwenye brenda usage upate mchanganyiko mmoja.
NA KWA UPANDE WA MATUMIZI
Osha nywele zako kwanza zitakate na baada ya hapo zikaushe kisha
paka mchanganyiko wako kwenye ngozi acha kwa muda wa dakika 20-25 kisha osha
kwa kutumia shampuu unayotumia ambayo unaamini ni nzuri.
Tumia tiba hii kwa wiki mara tatu utaona jinsi utakavyokomesha
moja kwa moja tatizo la mba kichwani.ukiona tatizo limezidi pata ushauri wa
daktari…
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv