karibu
msomaji wa edonetz leo tujifunze kuhusiana na jinsi ya kujua siku za mwanamke
za hatari za kubeba mimba ni zipi lakini watu wengi wamekua wamekuwa hawaelewi
basi fuatana nami kwa umakini zaid twende kujua hizo siku za hatari kwa
wanawake
Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni
siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila
wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume
wake ana matatizo.
Utazijuaje siku hizo?
Kwanza
kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako.
Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35,
mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio
mzunguko ambao watu wengi wanao.
Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu
siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla
ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu
mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako
haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni
vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko
zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28..
maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.
Je siku za hatari
ni zipi?
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.
Mfano
kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni
siku ya 14,
lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike
linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla
na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.
Kama
mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni
hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.
Kama
mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21
ukatoa 14 unapata
7
yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto
wa kiume] na 8.
Dalili
kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Kuongezeka
kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..
HITIMISHO
maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga
uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote
nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka ndio za mtoto wa kiume
zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv