Ni kawaida kwa wanawake kuwa na nywele kifuani; hizi humea wakati wa kubalehe. Hata hivyo, wakati mwingine nywele hizi huwa nyingi kupita kiasi tena kote kifuani kutokana na kasoro za homoni mwilini.Nywele hizo humea kwenye chuchu na huwa nyeusi zaidi kuliko nywele za sehemu zingine mwilini.
unayostahili kufahamu Haya hapa kuhusu nywele kumea sehemu nyeti
Ni sawa kuwa na nywele kwenye kifua
Ni sawa kuona nywele kifuani wakati wa kubalehe, uja uzito, kukatika kwa hedhi ama kutokana na kasoro za homoni. Hata hivyo, kuna nyakati ambapo nywele hizo huashiria tatizo: zinapomea kutoka kwa chuchu, zinapomea kwa kasi sana ama kwa wingi. Itakuwa vyema kumtembelea daktari.
Jinsi ya kuondoa nywele kifuani
Kuna njia nyingi kadha; kuzing’oa kwa kutumia kikoleo ama kuzikata kwa makasi. Vile vile unaweza kuonyoa, ingawa unashauriwa kuwa hufai kamwe kunyoa chuchu bali nywele tu zinazozingira eneo hilo, tena kwa uangalifu mkubwa.
Iwapo nywele hizo bado haziondoki na zimeanza kukuletea mafadhaiko, inapendekezwa umtembelee sdaktari ambaye atafanya operesheni ndogo ya kung’oa nywele hizo ama kuondoa kitu kinachochoea kumea kwazo.
Jinsi ya kubaini iwapo nywele ni nyingi kupita kiasi na sio za kawaida
Iwapo nywele zinamea kwa kasi, ni nyingi na zinakukwaruza hii ni ishara ya kuwepo kwa homoni ya kiume kupitaa kiasi mwilini mwako. Tatizo hili hufahamika kama Cushing’s Syndrome na hutokana na homoni ya Cortisol.
Homoni hiyo yaweza kusababishwa na uvimbeuchungu ama kumeza dawa zilizo na kemikali za Steroids. Usisite hata dakika moja, fika kwa daktari!
Ugonjwa wa Polycystic Ovarian Syndrome
Kasoro hii husababisha nywele kumea kwa wingi kifuani na vile vile sehemu zingine za mwili. Isitoshe, mgonjwa huwa mzito kupindukia, hutumbukia katika mafadhaiko na nywele huanza kutoweka.

Kumbuka kujikagua vizuri kifuani; iwapo ni nyuzi kidogo tu za nywele hamna la kukutia wasiwasi. Hata hivyo, iwapom mambo ni tofauti fika haraka kwa daktari.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top