miongoni mwa vitu vinavyoweza kuibadili dunia
ni mitandao ya kijamii haswa Faceebook Twitter, Instagram pamoja na Snapchat.
Kila mmoja anaitumia vile awezavyo na hapa sasa tuone watu wanaomiliki mitandao hiyo na utajiri wao
.
mtandao Instagram ndio unatoa hela ndefu katika watu wengi
kupata matangazo watu ambao waliokuwa na wafuasi wengi yaani ‘Followers’ wanapiga pesa sana japo
mitandao mingine pia inapiga pesa .
1.KEVIN SYSTROM
Huyu ndiye mmiliki halali wa mtandao wa Instagram
ambapo aliizindua Oktoba 6 mwaka 2010, na moja ya sheria za mtandao huu
hauruhusiwi kuufungua ukiwa chini ya miaka 17 hivyo kama unataka kufungua
ukurasa huu lazima uwe na umri kuanzia miaka 18. Kevin ana utajiri wa wa dola
za kimarekani 1.1 Bilioni.
2.MARK ZUCKERBERG
Wale watu wa mtandao wa Facebook ambao umetupa
jeuri sana na ndio mtandao namba moja uliowateka wengi na bado unawateka wengi
haswa kwa aina yake ya uungwaji wa picha na vitu mbalimbali
vinavyopatikana humo. Wakati inatoka tulifurahi sana mimi nimejiunga na mtandao
huu mwaka 2009 sasa utaweza kujiuliza mtandao huu uliundwa mwaka gani ?
Facebook imeanzishwa February 4 mwaka 2004 na huyu ndiye mwenye pesa ndefu sana
miongoni mwa wamiliki wa mitandao hii ana utajiri wa dola za Marekani 55.3
Bilioni.
3.JACK DORSE
Huyu naye ndio mmiliki wa mtandao wa Twiter mkazi
wa Marekani , huu unaaminika kuwa mtandao unaowakilisha watu wanaojielewa haswa
wengi wanatumia mtandao huu ku-Tweet na kupashana habari mbalimbali jamaa anamiliki
mtonyo wa Dola za Marekani 1.2 Bilioni hadi kufukia mwezi wa nane mwaka huu.
wapo na wanaomiliki
mitandao mingine kama Imo Skype pamoja na Snapchat basi kaa nasi ili
ujue mengi yanaendelea duniani. Ila kwa ufupi hii ndio mitandao inayofanya vizuri
sana duniani.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv