Kutoa huduma ya kwanza ni mhimu sana kwa binadamu wa kawaida na
kutoa huduma ya kwanza sio kitu kigeni kwa walio wengi wanaelewa vizuri tu na Watu wengi sasa wana ujuzi wa huduma ya
kwanza, wakikutana na hali ya dharura huwa hawahangaiki kama zamani. Lakini
njia zisizo sahihi wanazotumiwa zinaweza kuharibu miili yao. Yafuatayo ni
makosa wanayoweza kufanywa wakati wa kutoa huduma ya kwanza, hivyo kama mtoa
huduma unapaswa kuyaepuka.
1.Kuinua
kichwa wakati pua ikitokwa na damu,
wataalamu wa masuala ya afya wanaeleza kufanya
hivyo kunaweza kusababisha damu kutiririka na kuingia kwenye koo na kusababisha
ukosefu wa hewa. Inashauriwa endapo utatokwa na damu puani baada ya kujeruhiwa,
usitumie vitu vyovyote puani kuzuia damu hiyo kutoka, kwani ukifanya hivyo
inawezekana ukasababisha ubongo wako kuambukizwa na virusi.
2.
Usitumie dawa ya meno unapoungua,
watu wengi wakiungua, wanapendelea kutumia dawa ya meno
kupunguza maumivu, hii ni hatari sana tena usijaribu kabisa kuweka dawa ya
meno juu ya sehemu uliyoungua kwani endapo utafanya hivyo unaweza kusababisha
mahali palipoungua kuambukizwa na virusi. Njia sahihi inayoshauriwa kufanyika
ili kushughulikia tatizo lililojitokeza ni kutumia maji baridi kusafisha na
kupunguza digrii ya joto sehemu iliyoungua.
3.Usimwinue
kwa haraka mzee aliyeanguka,
kusaidia wazee walioanguka kusimama mara moja ni hatari
sana, wanasayansi wanasema mifupa ya wazee wengi huvunjika kirahisi
na huchukua muda pia hadi kujiunga na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Endapo utahitaji kutoa huduma ya kwanza kwa mzee aliyeanguka unashauriwa
usimfanye asimame mara moja (kwa haraka) kwani anaweza kujeruhiwa zaidi.
Hivyo ukikutana na mzee aliyeanguka na ukishuku kwamba
amevunjika mifupa yake, bora usimwinue mwache na usubiri gari la wagonjwa,
lakini akitokwa na damu, bora umsaidie kuzuia kutoka na damu kwanza
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv