Wanawake walio wengi wanalalamika kila kukicha wakidai wapenzi
wao wanawakimbia hila mimi naweza kusema kabla haujasema umekimbiwa kwanza
angalia wewe umemfanyia nini mpaka ulalamike na Unaambiwa raha ya penzi ujue
kuenzi, Je mpenzi wako unamfurahisha kwa mambo yapi? basi leo nikuibie siri
Jinsi ya Kumfurahisha Mwanaume wako katika mahusiano yenu.
KUWA KARIBU NAE,
Unapoanzisha uhusiano ujue kabisa kile ni kitendo kisichokuwa
cha hiari jitahidi mara moja moja unamridhisha mwenzi wako sio kila siku uko
bize na shughuli za hapa na pale wenzio wakichangamkia fursa ujue itakula kwako
na usiposhtuka mapema utajikuta unasubiri Meli Airport.
ISHI NAE KWA AMANI,
Kuna watu wanajikuta wanataka kubembelezwa tu pasi na sababu
atatafuta sababu ilimradi tu atake kujua kwamba akimuudhi mpenzi atachukua
uamuzi gani, angalia kuna wengine hawajui kubembeleza kwa kingereza tunawaita “unromantic men” yaani huyu
ukimzingua tu inakula kwako.
USICHUNGUZE SIMU YAKE,
Mahusiano ya kipindi hiki cha utandawazi yamegeuzwa thamani yake
kuwa ni sawa na utamu wa bazoka unatafuna ikiisha utamu unatema lakini chanzo
cha yote ni simu za mkononi kwani zimechochea sana usaliti hasa huu mtandao
ulioteka vijana wa sasa “Whatsapp” mtu akitumiwa
picha tu hata mtu hujawahi kumuona ushaingiwa tamaa. Ili kuepukana na presha
zote hizo achana na kukagua simu ya mwenzi wako yaani kwa lugha nyepesi acha
shobo na simu ya mwenzio maana isije kuwa chanzo cha kuhatarisha uhusiano wako
na wanaume wengi hawapendi kwa kuzingatia hilo atakupenda mno.
MLISHE AU JENGA MAZOEA YA KULA PAMOJA NAE,
Hivi wewe hapo ukilishwa huwa unajisikiaje? Bila shaka jibu ni
raha tupu asikwambie mtu mwanaume ni kama mtoto jitahidi kuenda nae sawia kwa
mahaba haya akikuacha basi huyo ujue kivuruge. Kuna wengine hudai kuwa
wanaostahili kulisha ni wale wanaotembea na waliowazidi umri la hasha! Utafeli
dada wewe utaishia kuambiwa niko bize na kazi tutaonana wikiendi.
USIMSUMBUE NA MIZUNGUKO YAKE,
Kuna wanawake wengine huwa wanaboa sio siri kwa hili badilikeni
mtu atataka ajue unaenda wapi na unafanya nini na uko na nani tena wengine
hufika mbali “ooohooo uko na nani
mbona huongei kwa kujiachia hebu ni kiss nijue kama hauko na mwanamke” tambua yule ni
mtu mzima anamajukumu yake sio kila kitu akwambie vingine kubali vikupite
asikudanganye mtu mwanaume hapendi kufatiliwa kupita kiasi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv