Asee!!!!! Unajua Kuna watu duniani wameumbwa kama vituko yaani ukimuangalia tu unaweza ukacheka watu hao wapo, yaani yeye ameumbwa kuchekesha tu mfano ukimuangalia Charlie Chaplin huyu ukimuona unyoaji wake wa sharubu lazima ucheke.
Rowan Atkinson ndio jina lake halisi amezaliwa 6 Januari 1955  pale Durham England wengi hupendelea kumuita Mr Bean , amepata umaarufu tangu alipo ingia katika kazi hizi za filamu haswa upande wa Vichekesho ama ‘Comedian’  kazi zake za awali kabisa ilikuwa ‘Not the nine Oclock News’ mwaka 1979 hadi 1982 pamoja na ile aliyoigiza kama polisi ambaye anaficha siri baada ya hapo amepata umaarufu mkubwa sana.
Watoto huwa wanampenda kama ilivyo Tom na Jery kuangalia vile vichekesho vyake, aina yake ya uchekeshaji anaumia vitu halisia katika kuchekesha sio vya kufikirika yaani anafanya vitu unaona . Bean ana mke anayeitwa Leslie Ash ambapo alimpata mwaka 1980 sasa sipati picha wakati anamtokea sijui ilikuwaje sijui alienda kama utani pamoja na hayo ana watoto wawili lakini waliachana  na mke huoy wa zamani, sasa yuko na tunda lingine Louuse Ford ambapi walianza mwaka 2014.

Inasemekana amestaafu mwaka 2012 aliliambia Telegrah kuwa amwchoshwa na mwili wake sasa umechoka hivyo anahitaji apunzike na tayari amefanikiwa vyakutosha , hivyo bado anapiga pesa kupitia matangazo mbalimbali ya Television 

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top