Kuna wakati tunalazimika kusema uongo ili
kunusuru jambo Fulani na matokeo yake inakuwa vizuri ila kuna wakati kusema
uongo kunaweza kuleta mkanganyiko na migogoro mingi sana katika jamii
tunamoishi sasa leo karibu tuone mambo ambayo wanawake upenda sana kudanganya. Na
jua sio raisi kukubali haya, lakini kuna aina ya wanawake ambao ni waongo sana,
na hiyo inajulikana, hata kuwashinda wanaume ambao inajulikana wao ndo wajanja
katika kudanganya kuliko wanawake, lakini leo tutaangalia vipengele ambavyo
wanawake wengi huwa wanadanganya sana.
Umri
Wanawake wengi wanaamini wanaume wanavutiwa
na wanawake wenye umri mdogo, wanawake walio na miaka kati ya 24-29 mara nyingi
huwa wanashusha miaka 2 hadi 3 ili waonekane wadogo mbele ya wanaume.
Kutokuwa Na Mahusiano
Baadhi wa wanawake, husema wapo kwenye
mahusiano hata kama hawapo,hii inatokea hasa kama mwanamke hamtaki mwanaume
aliemtokea wakati huo na kisingizio kikubwa ni yeye kuwa katika mahusiano na
huu ni uongo mmoja maarufu sana na Baadhi ya wanawake pia huwa wanaficha kama
wapo kwenye mahusiano, hasa pale wanapotaka kuanzisha ,mahusiano mapya, huku
wakiendelea kuwa na mahusiano na wanaume wawili kwa wakati mmoja.
Mara ya mwisho kukutana kimwili na mwanaume
Mwanamke hawezi kukwambia ukweli kuhusu hili
hata kama alikutana na mtu kimwili jana, atakwambia miezi 4-8 iliyopita, hii ni
kwasababu anaona ataonekana muhuni sana au Malaya, na wengi wao huwa wanataka
kuonekana wasafi au tuite watakatifu. Kitu ambacho sio
Ameshakuwa na wapenzi wangapi
Uongo mwingine ambao ni maarufu ni kuhusiana
na mwanaume wangapi ametoka nao, hapa sahau sana kwani huwezi kupata jibu
sahii, sababu wanawake wengi huwa wanadanganya mahusiano yao ya nyuma, anaweza
kukwambia wawili au watatu kitu ambacho inaweza kuwa zaidi ya hao. Japokuwa uongoo
huu hata wanaume pia wanadanganya
Kudanganya kuhusu vitu alivyozoea
Wapo wanawake wanadanganya kuhusu kutoka
usiku, labda sio watu wa tungi/Gambe, sio watundu kitandani na kujidai ndo
kwanza kuna mambo wanayaanza siku hiyo. Kujidai hawawezi hiki mara kile mara
akwambie mie ndo mara yangu ya kwanza ilimladi vituko .
Ila kitu kimoja ambacho nimegundua mwanamke
mpaka anafikia stage ya kudanganya haya ni kwa sababu ana mapenzi ya dhati na
mtu huyo na anaogopa kumpoteza kama akijua baadhi ya vitu vyake vya ndani.
Japokuwa wakati mwingine hali hii haijengi bali inabomoa mahusiano.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv