ukianza maisiano yako vizuri basi tarajia kuendelea vizuri na mahusiano yako kwani jambo jema uanza vyema wahenga walisema siku njema uonekana ahsubuhi ,basi kutokana na hili nikaona bora nikuletee vitu mhimu vya kuzingatia unapoanzisha mausiano..
KWA WATARAJIWA
1.Muonekano.
Usidanganyike na muonekano wa nje au yale maongezi ya mwanzo. Kila mtu hua mstaarabu siku za mwanzo hata wale ambao hawana ustarabu.
2.Usikimbilie kutangaza nia haraka.
Siku zote ni rahisi mtu kua muwazi kwa rafiki yake kuliko kwa mtu ambae anajua anataka mahusiano nae kwa hofu ya kumpoteza.Tumieni muda wakutosha kufahamiana kama marafiki kabla hamjajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi.
3.Uliza maswali kuhusu vitu ambavyo ni muhimu sana kwako.
Unapoanzisha mahusiano mapya inabidi ujue vitu muhimu kutoka kwa mwenza wako.Kwa mfano kama ni mtu wa familia au sio.
4.Penda kujua malengo yake ya baadae.
Hii itakuwezesha kugundua ni mtu wa aina gani,kama ni mpenda maendeleo,mtu wa starehe tu n.k.
5.Kuwa muwazi.
Hii inakwenda kwa pande zote,kuna vitu ambavyo ukimwambia mtu ni vidogo sana ila ukificha vinakua na kusababisha migongano kwenye mahusiano.
6.Hakikisha uwezo wenu wa kuelewa unaendana.
Hapa siongelei darasa ila mnavyokua sambamba kwenye maongezi ya kawaida tu yasiyo hitaji degree.
7.Onyesha misimamo yako hata kama unaona ni migumu kueleweka. 
Ni vizuri mtu akikubali, kujiingiza kwenye mahusiano na wewe awe akijua atakua na mtu wa aina gani. Kama hupendi nguo fupi, mwanamke/ mwanaume mnywaji wa pombe, mvuta sigara n.k inabidi mwenza wako ajue ili aanze kujirekebisha mapema ili kuepusha mizozo.
8.Hakikisha kuna vitu mnavyoshabihiana.
Kabla ya kuingia kwenye mahusiano inabidi uchunguze vitu ambavyo mnaendana ili kuimarisha ukaribu wenu ili kuepusha kila mtu kwenda na njia yake.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv


 
Top