Miongoni mwa vitu vinavyofanya watu waishi maisha mazuri sana
duniani ni vipaji walivyo jaaliwa na mwenyezi mungu na inakuwa furaha sana pale
unapoishi ndani ya ndoto yako kutokana na kipaji ulichopewa kwanza jiulize
yafuatayo wazazi au walimu wako wameshawahi kugundua uwezo wako katika kipaji
cha jumla mfano taaluma, michezo, kuzungumza, nk? Ulishawahi kujulishwa au kupata tetesi? mpaka sasa kipaji hicho kimeshajitokeza na kukufanya uwe na mahala
pamoja unapofanya vizuri zaidi ? kama ndiyo tumia fursa hiyo kipaji
kitatokeza.
Chunguza
mazingira yako,
angalia mazingira ya unachofanya kama yalitokana na uwezo wako
wa asili au ulijiingiza kwa kuhamasishwa na mtu, shida, au tamaa ya kutajirika
haraka. Tafuta kile kinachotokana na uwezo wako wa asili ili kipaji chako
kiweze kufanya kazi.
Angalia
ulichokuwa unakifanya,
angalia kama kuna ulichokuwa ukikifanya hapo zamani ambacho hata
kama hukukifanya kwa ufanisi kwa kukosa maarifa lakini kilikupa upekee lakini
kiwe kilitokana na uwezo wako wa asili na ulifanya mara kwa mara. Kiendeleze na
baada ya muda kitakupa mwelekeo wa wapi uende na hivyo kufanya uwe tofauti na
wengine.
Nini
kilikutambulisha na kinachokutambulisha,
angalia katika unavyovifanya au ulivyovifanya ni kipi
kilikutambulisha au kinakutambulisha na kukufanya ukubalike kipekee na sio
kutokana na kiwango chako cha kisomo. Kipaji halisi hakitegemei kiwango cha
kisomo, bali uwezo wa asili ndio hutawala katika kutenda jambo. Katika kiwango
chochote cha elimu bado uwezo wa asili utachukua nafasi na kutawala katika
utendaji na kukufanya wewe ndiyo upate sifa na sio elimu yako.
Ni nani
aliyekwambia una Kipaji?,
jiulize kama umeshawahi kuambiwa una kipaji? Je ni kipaji gani?
Umeshawahi kuambiwa mahala kwingine na hapo maneno kama hayo? Hicho ndicho
unachokifanya mara kwa mara kwa ufanisi kuliko mengine?.
Tazama
hisia zako,
angalia kama unachofanya unahisia nacho au unafanya kwa sababu
hauna kazi nyingine? Na hisia zako za ndani zinasemaje? Jali zaidi hisia zako
za ndani sana zinazohusiana na uwezo wako bila kujali vitisho kwa sababu kipaji
kina nguvu kuliko kitisho chochote kilichoko mbele yako.
Kama wewe hujawahi kuhisi au kusikia chochote kuhusu kipaji
chako basi ni kwa sababu ya kukosa nafasi ya kukionyesha. Fanya kila unachohisi
kinatokana na uwezo wako wa asili hata kama kimewahi kufanywa na mtu mwingine
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv