Mama anapomaliza first trimester (miezi 3 ya mwanzo) tumbo
linaongezeka ukubwa kutokana na ukuaji wa mtoto. Ukuaji wa mtoto unadhiri
pisition ya ulalaji wa mama,hivyo mama anashauriwa mimba ikifika miezi 4
(wiki 16)asilalie tumbo au mgongo.
MAMA
ASILALIE TUMBO AU MGONGO
Kulalia mgongo sio vizuri kwa sababu uzito wa mtoto unazuia
baadhi ya mishipa ya mgongoni inayosafirisha damu toka kwenye uti wa
mgongo kwenda kichwani,na kutoka miguuni kuja kichwani kushindwa
kusafirisha damu vizuri na kunabadili mfumo wa mzunguko wa
damu unaoweza kumuadhiri mama au mtoto.
PICHA INAONYESHA MAMA AKILALIA TUMBO
,JINSI MTOTO ANAVYOLALA VIBAYA ,NA PICHA YA PILI MTOTO ANAJISIKIA VIZURI
MAMA ANAPOLALIA UPANDE WA KUSHOTO.
Adhari atakazo zipata mama mjamzito
atakapo lala kwa mgongo (chali) / kulalia tumbo
Kutokana na damu kushindwa kusafirishwa vizuri inapelekea
kumsababishia mama mjamzito kupata matatizo kama,
:Kuvimba kwa misuli na inayo ambatana na maumivu (miguu na
mikono)
:Kushuka au kupanda kwa blood pressure
:Ini kuelemewa uzito
:Kupunguza mzunguko wa damu ambayo ni hatari kwa uhai wa mtoto
:Kusikia kizunguzungu mara kwa mara
:Mama kupata kiungulio mara kwa mara nyakati za usiku
:Kukoroma
:Maumivu ya mgongo
:Mama na mtoto ushindwa kupumua vizuri kwa kusosa hewa (oxygen)
:Mtoto kukosa virutubisho vya kutosha.
Mama anatakiwa alalie position gani ili
awe salama?
Tafiti nyingi zinamshauri kwamba mama mjamzito
alalie upande wa kushoto .Sababu damu husafirishwa kwa Urahisi
zaidi kutoka kwenye moyo wa mama na kwenda kwenye kondo la
mtoto na kumpa virutubisho vingi zaidi. .
Iwapo mama atalalia tumbo au mgongo itamfanya mtoto asiwe comfortable
atahangaika na kumpiga piga mama ili abadili position ya kulala.
USHAURI
Mama anapolala ni vizuri akaweka mto katikati ya miguu
usibane miguu ipitanishe, inakusaidia kulala comfortable,damu kusafirishwa
vizuri na kutopata maumivu ya mgongo.Nyakati za usiku ni kawaida kwa
watoto kupiga piga tumboni ,ila akipiga sana jua umelala vibaya
anataka ubadilishe position.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv