Aliyekuwa
Spika mstaafu wa Bunge na Waziri Mwandamizi Mhe. Samuel Sitta amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo huko Ujerumani akiwa katika matibabu... Poleni ndugu ,
jamaa na marafiki wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi
Amina.
NA kwa upande mwingine..Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job
Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo
Tabora Samwel Sitta.
Mzee
Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical
University of Munich Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi
uliopita.
Katika
salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa
taarifa za kifo cha Samwel Sitta na Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa
mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.
“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na
tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika
ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.
“Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa
Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia
nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.
Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki
kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.
“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema
peponi, Ameni”
Taarifa imetolewa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano
ya Rais, IKULU. Dar es Salaam
NITAZIDI KUKUJUZA JUU TA HILI ..................