Mtandao wa Wikipedia umekataa kufuta picha ambayo Nyani ilijipiga ikisema kuwa kwa sababu picha hiyo ilipigwa na Nyani ambaye ni mnyama wala sio binadamu, basi inakuwa mali ya umma.

Hii ni baada ya mpiga picha, mmiliki wa kamera iliyotumika na Nyani huyo kujipiga picha, kusihi Wikipedia kufuta picha hiyo na kudai kuwa Wikipedia ilikuwa inaingilia haki zake za umiliki wa picha hiyo.

Mpiga picha, David Slater, alikuwa akijaribu kunasa picha za Nyani kwa masaa kadhaa, wakati ambapo Nyani mmoja alichukua mojawapo ya kamera za David na kujipiga mamia ya picha.

Picha hiyo aliyojipiga Nyani bila shaka ni ya kusisimua na imempeleka David kuwa maarufu ulimwengu mzima.


La kusikitisha ni kuwa hatimaye Slater sasa amejipata katika mvutano wa kisheria na Wikipedia kuhusiana na ni nani hasa mmiliki wa picha hiyo.
 
Top