Kila siku nakuletwa makala mbalimbali za mahusiano
siasa afya michezo na kila kitu leo nakukaribisha ushuudie umuhimu na faida 4
za kumbatio (hug) katika mapenzi….
HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA
Unapomkumbatia mkeo ama mpenzi wako mkiwa mmelala husaidia
kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho ‘oxytocin’. Homoni hii hufanya
kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na hupunguza
shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa
na maumivu ya kichwa na maradhi mengine.
USINGIZI MARIDHAWA
Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti
mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza ‘cortisol’ na hivyo
hupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi ‘cortisol’ inapopungua mwilini,
moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.
Unapomkumbatia mwandani wako huleta raha, hasa mambo
yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya
mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… moyo wako unatakiwa
kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na
hisia za ushirika.
MAWASILIANO BILA MANENO
Kukumbatiana hutoa fursa kwa wapenzi ya kuwasiliana bila
kuongea. Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa
karibu.
NI DAWA YA FADHAA
Kimbilia kitandani ili kupata kumbatio la asali wako wa moyo;
kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na kitabu, televisheni,
simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika
na kupata utuvu.
HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA
Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kweye tendo la
ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti
mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na
ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv