Kumtokea mwanamke ni suala ambalo linaitaji ustadi mkubwa hili lengo lako litimie wengine ukurupuka na kujikuta wanaangukia pua na kujiona hawapendwi hila ukweli ni kwamba hawajafuata kanuni … Kama unataka kumpata mwanamke unayemzimia bila tatizo lolote basi hakikisha unafuata taratibu hizi,  kwani utapata ujasiri wa kumtongoza mwanamke, kuanzia siku ya kwanza hadi anapokuwa wako.
Angalia ishara. 
Ufunguo wa kutongoza ni kuzijua na kuzivumbua ishara kwa yale anayofanya na kutenda, kuwa makini na stori ambazo anaeleza, mambo ambayo anapenda kuongea na kila kitu ambacho kinaamsha hisia zake. Kumbuka hapa unakuwa makini kwasababu ya mwanamke na wala si wewe hivyo usijaribu kutoa maoni  yeyote bila kufikiria madhara yake.
Cheza na hisia zake. 
Hapa jambo muhimu la kufahamu ni kuwa ni vyema uchague maneno matatu yenye ushawishi ya kumwambia mwanamke, unaweza kubadilisha hisia zake na akakubaliana na matakwa yako, Huu uwezo wa ‘kubadilisha’ hisia za mwanamke ni jambo muhimu zaidi ya yote ikija katika maswala ya kumtongoza mwanamke.
Mpe uhakikisho. 
Kila mwanamke (hata kama ni mrembo kiasi gani ama ‘amekamilika’ mbele ya macho yako) huwa wana hulka ya kutojiamini ndani yao ambapo kunahitajika kupewa uhakika kwa njia moja au nyingine. Hivyo, jambo muhimu la kuzingatia wakati unampa uhakika ni pale ambapo utakuwa mkweli.

Kumwambia kuwa ana macho mazuri hakutasaidia; hii ni kwa sababu maneno kama haya yashatumika mara kwa mara na kila mwanaume anatumia maneno hayo hayo. Kumpongeza na kumpa na kumuhakikishia kwa jambo ambalo hajiamini nalo kutamfanya akuthamini na kumuweka karibu na yeye zaidi na kama umefuata hatua hizi mbili za kwanza vizuri basi hautakosa kupata jambo ambalo litampendeza.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone 
 
Top