Pale unapozama penzini unatakiwa kuwa makini
ili Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni vigumu, lakini hizi
mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe zitahakikisha umesimama na
yeye madhabahuni haraka sana.
Kuwa girlfriend kamili.
Kinachotakiwa Nyote wawili mumeinjoy maisha ya furaha,
mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba una uwezo wa kumwambia kila kitu
ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo na ufikirie mambo ambayo unaweza
kufanya zaidi ya hayo.
Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama
na special, haya ndio mambo ambayo anahitaji zaidi. Bila shaka utakuwa unamjua
zaidi ya mtu yeyote yule. Kile ambacho anapenda na kuchukia, na mambo ambayo
yatamfanya akuone kuwa wewe unapendeza zaidi ya kitu chochote kile.
Hakikisha unafanya kila kitu ambacho mwanamke
kamili anaweza kufanya. Mwonyeshe kila kitu ambacho anahitaki, na bila shaka
atakuona wewe umejitweka jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili
yake.
Jifunze kumtunza.
Mfanye mwanaume ahisi kuwa hawezi kuishi bila
wewe, basi bila shaka atahakikisha ametia kufuli jambo hilo. Hakikisha kuwa
unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo madogo madogo, hata kama ni jambo
rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama kumpa sapoti wakati anapohitaji.
Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko ya haraka sana, na hatoweza
kustahimili kuishi bila wewe.
Kuwa shabiki wake mkuu.
Unatakiwa kuwa shabiki mkuu wa mwanaume wako. Kitu chochote
kile ambacho ayaamua kufanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha
wewe mpe sapoti kwa kumshabikia atimize azma yake.
Ile siku ambayo atakuja kugundua kuwa
mafanikio yake katika azma yake yamechangiwa na wewe basi atakuweka karibu
yake. Atakuona kuwa wewe umekuwa karibu yake bila hata kupoteza imani katika
azma yake.
Mtreat.
Wakati mwingine wanaume huchoka kwa kuwa wao
ndio kila wakati huwatoa wanawake out na deti. Msaprize siku moja kwa kumtoa
out siku moja, na kuhakikisha unafanya mambo ambayo anapenda kufanya.
Tumpeleka sehemu romantik, kumtoa katika
dinner na kumuonyesha jinsi romance inavyokuwa kutamfanya achangamke na labda
anaweza ingiwa na jazma ya kukutamkia lile neno ambalo umekuwa ukilingojea
kutoka kwake kwa miaka.
Kuwa mkweli kwa kile unachotaka.
Wanaume wengi si wajuzi wa kusoma akili ya
mtu. Wakati mwingine unaweza kuwa katika mahusiano na mwanaume kwa miaka mingi
na ukashangaa ni kwa nini mwanaume kama huyu hajakuposa. Kuna uhakika mkuu ni
kuwa wazo kama hilo bado halijamlenga kwa kichwa chake.
Kama umekuwa na maongezi ya ukweli na
mwanaume wako, na ukaweka wazi kuwa unampenda, na ukaeleza vile ambavyo unaona
mahusiano yenu yatakuwa miaka inayokuja, basi anaweza kuingiwa na hali ya
kutaka kuchukua hatua ya mbele kuhusiana na unavyosema. Hata kama hana uhakika
na ndoa, atleast utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.
Usiwe comfortable sanaa.
Kuwa comfortable sana katika mahusiano ni
hatari sana. Haswa iwapo kama unataka mwanaume wako achukue hatua ya mbele. Ni
rahisi kujisahau katika hali ulioko wakati huo na mwishowe kuwa mvivu. La kufanya
ni kuhakikisha kuwa unatafuta maisha yako wewe mwenyewe, interests zako na
marafiki wa kwako.
Hakuna kitu kizuri zaidi kama mwanamke ambaye
ana uwezo wa kujitegemea mwenyewe. Mfanye akuone kuwa wewe una mambo yako
ambayo unafanya, na kuwa una maisha yako ya nje kando na kuwa katika mahusiano.
Soon ataanza kuona jinsi ilivyo rahisi kwako kuenda zako, na hivyo atahakikisha
ya kuwa jambo kama hilo halitokezei.
Usimuogopeshe.
Usimuogopeshe mwanaume ili akupose kwa kuwa
hilo si jambo la kufuata. Inakubalika kuongea maswala ya ndoa, na kueleza
msimamo wako. Lakini iwapo utakuwa kila wakati unamtia presha, kila wakati
unagusia swala la ndoa, ama kuanza kutokwa na machozi kila upitapo mbele ya
duka la harusi basi utafanya ile dhana ya kwake kukuoa kufifia haraka sana
kwani atakuogopa.
Mwonyeshe kuwa wewe ni wife material
anayemwota.
Ukimwona mwanaume ameamua kuwa wewe ndie
aliyekuchagua basi tayari alikuwa alikuweka kwa ndoto zake awali.
Kama unamtaka aweke pete kwa kidole chako,
basi mwonyeshe kuwa wewe utakuwa mke mwema. Kuwa mtiifu, mwaminifu, mpole,
mvumilivu, na mpendezi. Muda si mrefu ataona kuwa hakuna mwanamke yeyote ambaye
anaweza kuzishinda tabia ambazo uko nazo.
Rudi nyuma.
Kama imepita muda mrefu na umeshajaribu mbinu
zote tulizozitaja hapo juu, basi jambo la mwisho ambalo unaweza kufanya ni
kurudi nyuma kiasi. Kumpatia mwanaume wako nafasi ya kupumua si jambo baya, Si
lazima ufanye mambo mazito ya kuleta atenshen ya bure. Kwa kupoa kiasi, anaweza
kuhisi kutokuwepi kwako na kugundua kuwa maisha yatakuwa hayana maana kama
hautakuwa na yeye.
Atagundua kuwa maisha yake ni mahumu bila
wewe na hapo hapo atakutaka uwe na wewe zaidi kuliko awali.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv