Karibu tujadili msomaji wa edonetz tujuzane na Haya ndiyo  mambo matano ambayo yanasababisha hali hii itokee na kumfanya mwenza wako aboreke kitandani na kuishia kutoa visingizio vingine visivyokuwa na maana sababu anaona aibu kukwambia.
Unaomba ruhusa
Kama ukiwa unauhusiano wa muda mrefu na mwanamke na umeshaelewa lugha yake ya mwili na hisia zake, hakuna kinachomuondoa kwenye hali ya kihisia kama kuombwa ruhusa ya kiofisi kuendelea na jambo hasa juu ya yale mambo yetu mazuri, hauhitaji karatasi ya mahakama ya ruhusa kuendelea kumpa vishawishi na kumtekenya. Mpenzi mzuri ni yule anayejua kumpa vishawishi na kumfanya asisimke kwa akshi hata kama akili haikua katika hayo mawazo.
Unatabirika
Kama mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, hii ndio litakuwa tatizo kubwa maana sababu ya kwanini mara ya kwanza mapenzi yalikuwa matamu kitandani kati yako na yeye ni kwa sababu ulikua hujui nini cha kutarajia. Kama ukiwa unataka kurudisha hali kama awali inakupasa ubadilishe ratiba na ufanyaji wa mambo ili kuleta hali fulani ya upya katika uhusiano wenu.
Usiogope kujaribu vitu vipya ambavyo wote kwa pamoja mnaweza kuvipenda, usiache ikafikia hali kiasi akawa anajua mpaka ni kitu gani utachokwenda kinachofatia unachokwenda kukufanya, kwa mfano kama huwa unatumia dakika 5 kumtayarisha kimapenzi, siku nyingine jaribu kabadilika na kutumia dakika 20.
Mapenzi ya kukurupuka
Mwanamke wako sio punda wa kupandwa bila matayarisho, hajawa doli la kuchezea. Wanawake wote hupendwa kutayarishwa na kupewa mapenzi ya huba yenye hisia, sio mapenzi ya kikurya “Mama Robhii, raraa nikurariie!”. Sio kwa staili hii jamaa, jaribu kuwa mvumbuzi wa mambo, ongeza viungo mtoto wa watu alegee na kusisimka kwa huba na mahaba, usiwe na haraka maana tayari yupo kitandani, mmenye kama ndizi kidogo huku unakula taratibu, kidogo tena huku ukiyaachanisha maganda taratibu na kwa staili ndo unakula tena, we ni mpenzi wake na sio mbakaji, mfanye akuone kama malaika uliyeshushwa toka mbinguni kwa kazi moja ya kumpenda na kumpa raha duniani.
Hujiongezi inavyopaswa
Japo wanawake wengi huwa ni rahisi kukubaliana na staili ya mapenzi kutokana na wenza wao, ila iwapo kama unatumia staili hio hio kila mkikutana na hamna vionjo vyovyote vinavyobadilika lazima mwenza wako achoke na kuboreka na utendaji wako wa kazi. Kwa hiyo kama ukitaka asikuchoke inabidi ujiongeze na ufanye mabadiliko ya hapa na pale. lazima ubadilike kimahaba, na sio kitandani peke yake hata nje ya hapo, mnong’oneze wakati mnapata chai ni nini utamfanyia giza likiingia, au mtumie meseji tata za jinsi unavyowaza na kutamani giza liingie uwe mikononi mwake, mtoe kwenye mtoko na mpe malavidavi ya kutosha na utamuacha anawaza umetokea sayari ipi.

Sehemu moja ya matukio
Kama mwanamke wako unampeleka sehemu moja tu ya tukio, mpaka amekariri basi fahamu kuwa upo kwenye matatizo makubwa. Ila mabadiliko ya uwanja yanaweza kutatua hili tatizo hivyo usiwe na wasiwasi,  jaribu kufanya matukio hata sehemu ambazo hategemei, mpeleke kwenye sofa, mpeleke bafuni na kama unamaji ya moto patakua patamu huko, itamfanya msichana wako akuone mtu wa masapraizi ya kutosha.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top