Utafiti unazidi kutuonyesha mambo mengi sana na hili ni jingine ambalo linaweza kutustaajabisha walio wengi ila ukweli ndio huu kutokana na utafiti ni kwamba Carlo Collodi ambaye ni mwandishi wa habari wa Italia aliyeandika hadithi ya mwanasesere aliyekuwa hai kama mtoto halisia, aliyetengenezwa na seremala mzee na  kumpa jina la Pinocchio kati mwaka 1881 hadi 1883. Lakini  mwanasesere huyo alipata tabia mbaya ikiwemo ya kusema uongo na kila alipokuwa akisema uongo pua yake inakuwa ndefu sana.

Hivi karibuni wanasayansi wa kitivo cha saikolojia cha Chuo Kikuu cha Granada cha Hispania wamegundua kuwa watu wanaposema uongo, huwa inatokea hali inayofanana na kwenye hadithi ya Pinocchio, yaani pua zao zinakuwa zamoto na ndefu zaidi. Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kupima joto wanapotafiti suala la kisaikolojia na wamegundua jambo hili la kuchekesha.

Licha ya kuongezeka kwa joto kwenye pua, misuli ndani ya macho pia inakuwa yamoto zaidi, na sehemu iitwayo Insular cortex kwenye ubongo pia inaanza kufanya kazi. Insular cortex inadhibiti hisia za binadamu, pia inahusiana na joto la mwili.


Mambo mengine pia yatasababisha mabadiliko ya joto mwilini. Wanasayansi wamegundua kuwa watu wanapofanya kazi ambayo inawahitaji kufikiri, nyuso zao zinakuwa baridi zaidi na wanapokuwa na wasiwasi nyuso zao zinakuwa zamoto.


JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top