Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba, dhana ya mapenzi
ina wigo mpana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja ‘TUMEPUMZIKA’ kuyazungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu
na kushauriana pale tunapohisi wengi hufanya makosa.
Hakuna kitu kinachoumiza katika uhusiano wa kimapenzi kama
kusikia mpenzi wako anatembea na mtu mwingine tena ambaye huenda
unamfahamu, inauma kupita maelezo; mbao wamewahi kusalitiwa wanajua
machungu yake.
Kwa kifupi kasi ya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa ikiongezeka
kila uchwao kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi
unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa. Hii ni kwa sababu watu
sio waaminifu kwa wapenzi wao.
Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza
kuwa, anakupenda, anakujali, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe
katika shida na raha. Lakini huyo huyo usishangae siku moja ukamkuta yupo
na mtu mwingine. Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini
wapenzi wanasalitiana?
Zipo sababu nyingi sana zinazowasukuma baadhi ya watu
kudiriki kuwaumiza wenza wao kwa kuchepuka nje ya mahusiano . Hata hivyo,
leo nataka kuzungumzia namna tamaa ya fedha na ya kimwili
vinavyochangia katika hili.
Kwa wale ambao wapo kweye ndoa wakati mwingine, hasa
wanawake wasipopatiwa mahitaji muhimu na akatokea jamaa na
kumhakikishia kumpatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua
kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga
mazoea.
Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa
kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta
wanatafuta waume wengine huku wakidai kuwa, wanatafuta ladha tofauti.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv