Siku zote unaweza kuchagua rafiki lakini huwezi kuchagua jiran na Kama Vitabu vya Dini vinavyoeleza kuwa ‘Mpende Jirani yako kama unavyojipenda’ pamoja na kuwa na msisitizo kwenye Vitabu vya Dini lakini bado kuna watu wanajaribu kuwapenda jirani zao na kuishi nao vizuri wanashindwa kutokana na utofauti wa tabia na mfumo wa maisha ya kila mmoja ingawa kuna wengine huwa hawa wathamini majirani wao na hii inawezekana ikawa kwa sababu ya kutokuwa na ufahamu juu ya faida ya kuishi na majirani kwa wema.
Leo tukae kitako tujadili juu hili ili tupate ufumbuzi zaidi ukiwa na chochote niandikie hapo chini kabisa hata kama utaitaji ufafanuzi juu ya mada Fulani niulize tu karibu..
Amani na upendo
Kuishi kwa wema na majirani ni amani tosha hasa kwa wale wanaojishughulisha na biashara au kazi, unapokuwa na mahusiano mazuri na majirani wako inakuwa rahisi kuacha nyumba yako na watoto wako kwani unakuwa umewaanza na watu unaowaamini.
Usalama
Majirani ni muhimu katika maisha ya mwanadamu kama ilivyo mwanadamu ana mitihani mingi  kwa hiyo pale unapoishi vyema inakuwezesha kuwa na amani kwani usalama wako na mali utakuwa kwenye mikono salama.
Ndugu wa hiari
Ukiishi vizuri na majirani unapata ndugu wa hiari kwani unaweza ukajikuta kwenye mazingira ambayo huishi na ndugu zako, karibu sasa pale utapokuwa na mahusiano mazuri na majirani husaidia kwani unapata ndugu wengine tofauti ili kukupunguzia unyonge na upweke.
Biashara
Ukiwa na majirani ni nafasi nzuri ya wewe kutengeneza pesa kwani kama ilivyosasa kwenye ulimwengu wa digitali kwenye upande wa biashara ya mtandao ambayo inahitaji mtaji wa watu kwa hiyo kupitia majirani watakuwezesha kukuza biashara yako kwani biashara ni kujuana.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv


 
Top