Katika mfurulizo wa makala nazokuandalia kila iitwapo leo makala
zinaangazia kila sekta, karibu edonetz leo tunaangazia baadhi ya changamoto kwa mpenzi
aliyekuzidi umri kama ifuatavyo
...Maneno maneno ya
kuvunja moyo kutoka kwa jamii
Inapotokea mwanamke akawa na miaka mingi sana kuliko mumewe jamii huweza kuongea maneno ambayo wakati mwingine huwakosesha raha na amani.

...Kukosa Uhuru wa
kuwa na Mwenzi wako Hadharani.
Kutokana na maneno ya watu mitaani, kanisani, kazini na kwingineko mnaweza kukosa uhuru wa kuongazana pamoja au kumtambulisha kwa marafiki au inapotokea mmealikwa kwenye sherehe au hafla fulani unapata utata wa kuongozana kutokana na kuhofia kunyooshewa vidole na watu kwa kuwasema vibaya.

...Kupishana kwa
mapendeleo na maslahi “Hobbies & Interests” Baina ya Wanandoa
Hao, Moja ya changamoto inayowakabiri wanandoa ambao wamepishana umri wa miaka
mingi ni kwamba mmoja atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa kiujana na mwingine
atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa Kiutuuzima au ulimwengu wa uzee. Tatizo
litakalotokea hapa kila mmoja anajaribu kumvuta mwenzake kwenye ulimwengu wake.
...Changamoto ya
Kutoendana na Kuangalia Nje ya “Fance”
Kadri miaka itakavyozidi kwenda ile “gap” ya umri itakuwa ikijitokeza kwa ukubwa zaidi. Kijana ataanza kuona huyu mzee hatuendani namimi yupo nyuma ya wakati na kuanza kuvutiwa zaidi na mtu mwingine wa rika lake. Mfano kama kijana ameoa mwanamke ambaye wamepishana sana umri, kijana anaweza kutamani mkewe awe anavaa yale mavazi ya ujana ambayo huvaliwa na wasichana mitindo na mishono ya kiujana ili atakapokutana na marafiki zake waone kuwa ana mwanamke ambaye anakwenda na wakati. Kwa upande wake huyo mwanamke kulinganana umri wake hawezi kuthubutu kuvaa mavazi ya kiujana kama hayo na hapo mgogoro huweza kutokea na wote wawili kuona kuwa hawaendani kabisa.

...Imani ya kwamba
Ndoa ni Kwajili ya Kupata Watoto
Katika tamaduni na mazingira yetu ya Kiafrika, umri wa mwanamke anapoolewa ni wa msingi sana hasa linapokuja swala la kuzaa watoto. Kwa tamaduni za kiafrika swala la kuzaa watoto katika ndoa ni jambo la msingi sana kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo mwanaume anapooa anakuwa na mategemeo kwa sehemu kubwa kwamba atapata watoto kupitia mke ambaye anamuoa.

...Jamii Huamini
kwamba Mwanamke Mwenye Umri Mkubwa Atashindwa Kuzaa.
Jamii nyingi huamini kwamba kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza kushindwa kumzalia watoto mumewe. Kulingaana na watafiti wanasema kwamba kadri mwanamke anavyoziku kuongezeka umri ndivyo ambavyo viungo vyake vya uzazi hupoteza uwezo wake wa kushika mimba na kuzaa watoto.

JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv