Ukiangalia
zamani na sasa hivi kila kitu kinabadrika na Kadri siku zinavyokwenda watu
wanahamasika kuachana na vyakula vinavyoweza kuongeza uzito mkubwa mwilini, ni
jambo jema kutambua madhara na kukabiliana nayo haraka kwani unene sio mzuri
hata kidogo. Hii ndio sababu siku hizi utakuta watu wanafanya mazoezi kwa kasi
sana ili kupunguza nyama zembe.
Kwa
kawaida mwili wa binadamu una mafuta ya aina mbili yaani mafuta meupe
ambayo yanatumiwa kuhifadhi nishati na mafuta ya kahawia ambayo yenyewe
huzalisha joto. Tafiti zinaonesha mtu mnene anaweza kutumia njia sahihi ya
kupunguza uzito kwa kufanya mafuta ya kahawia yazalishe joto jingi zaidi.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Leipzig cha Ujerumani wamegundua njia mpya ya
kupunguza uzito kupitia kupunguza mafuta kahawia.
Katika
miaka mingi iliyopita, wanasayansi waliona mafuta ya kahawia yanafanya kazi
nyingi zaidi katika miili ya watoto hivyo utafiti uliofanyika katika miaka ya
hivi karibuni unaonesha kuwa mafuta ya kahawia ndani ya miili ya watu wazima
pia yanaweza kuamshwa na baadhi ya mafuta meupe yanaweza kubadilishwa kuwa
kahawia.
Watafiti
walipofanya majaribio kwa kutumia panya, wamegundua kuna kemikali iitwayo Phosphodiesterase
10A
ndani ya mafuta ya mwilini. Kazi ya kemikali hiyo ikizuiliwa, mafuta ya kahawia
yataamshwa, baadhi ya mafuta meupe yanabadilika kuwa kahawia, uzito wa panya
utapungua kwa kiasi kikubwa na uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari
utapungua. Hivyo njia hii ikitumika itasaidia kupunguza uzito kwa watu wanene.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv