Karibu sana msomaji wa
edonetz na leo tujadili hili ,Kwa kawaida mama wakwe wanachukuliwa kuwa na utofauti
mkubwa utakuta wengine wana upendo anaweza kukufanya kama motto wake na wengine
wanakuwa kinyume kabisa wanaweza kusho sumu ya ndoa yako. Wakati huo huo kuna
wanawake ambao wanadai kuwa hawana uhusiano mzuri na wakwe zao, lakini kwa
chini chini wanatamani sana kuwa na uhusiano mzuri na mama mkwe. Kujua kama umo
kwenye kitabu cha moyo wa mheshimiwa mama mkwe,
basi hizi ndizo ishara na dalili za
kukuonesha hilo:
1.Anapokuulizia mara kwa mara:
Baada ya shamrashamra
za harusi iliyofana vizuri, mama mkwe anatulia huku akiwa mwenye furaha.
Anakupigia simu kuuliza hali yako. Anataka kujua lini utamtembelea. Kwa ufupi
unakuwa kama mwanaye kwake na moyo wake umejawa mahaba juu yako.
2. Anapokutembelea muda wowote:
Sio kawaida kwa mama
ambaye umri wake umesonga kufunga safari ndefu kutoka kijijini kwa ajili ya
kumtembelea mwanaye pekee. Wamama wengi wazee – isipokuwa wachache –
hawapendelei kuwatembelea watoto wao kwa sababu ya wake zao.
3. Anakutumia au anakuletea zawadi:
Anapokutembelea haji
mikono mitupu. Anakuletea yule jogoo mwenye kilo 7, kiroba cha mahindi, ndizi,
kunde na chochote kizuri kutoka kijijini. Usidhani kuwa hayo anayafanya kwa
sababu ya mwanaye wa kiume. Bali ni kwa sababu wewe mke wa mwanaye ni mke alimkubali
pia.
4. Anakupigania:
Mama mkwe anayekupenda
atakupigania na kukutetea kuhakikisha kuwa heshima yako haivunjiki. Hata ukiwa
na msuguano na mume wako, utaona anakuwa upande wako na kutuliza mambo.
5. Watu wako ndio watu wake:
Tangu ulipoolewa na
mwanaye, mama huyu amekuwa karibu sana na watu wako. Yuko karibu na mama yako
na shangazi zako. Hakosi shughuli za furaha na huzuni za familia yako.
6. Anataka usaidizi wako wa jikoni:
Kuna wageni wamekuja
nyumbani kwake, atakuuliza aina ya chakula ambacho ungependelea kipikwe. Hata
kama kuna wanawake wengine, bado atasisitiza ushiriki katika upishi. Mara
nyingi baadhi ya wanawake hulichukulia kwa mtazamo mbaya jambo hili, lakini
ukweli ni kwamba hiyo ni kama cheti unachopewa na mama mkwe.
7. Anapokuzungumzia vizuri mbele ya marafiki
zake :
Wamama wengine
wanapolalamika kuhusu wake wa watoto zao ambao wana muonekano mbaya, kucha za
bandia, nywele za bandia na wasioweza kupika chakula cha watu 20, mama mkwe
wako yeye anakusifia tu.
8. Anajawa na wasiwasi unapokaa kwa wazazi wako
muda mwingi
kupitia kiasi: Unapowatembelea ndugu zako na ukakaa huko
kwa zaidi ya siku moja, mama
huyo hukosa amani. Hujawa na wasiwasi kwamba yumkini umeitelekeza familia.
Haachi kukupigia simu kuuliza lini utarudi.
9. Anaheshimu ndoa yako na haingilii mambo yenu:
Hamuulizi mwanaye au
yeyote kuhusu mambo ya ndoa yenu. Anajiweka mbali lakini tatizo likitokea,
anakuwa wa kwanza kuja kuwasaidia.
10. Anakuona kuwa ni chaguo sahihi:
Mara nyingi mwanaume
ndiye anayefanya uamuzi wa kuoa. Lakini, anapomchagua mtu, mama hulazimika
kukubali. Mama mkwe anayekupenda huamini kwamba wewe bado ni chaguo sahihi hata
kama miaka mingi imepita tangu ulipoolewa. Hizo ni ishara zitakazokuonesha
kuwa mama mkwe anakupenda au la!.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv