Jamii
yetu imekumbwa sana na janga hili la utoaji wa mimba hasa kwa mabinti wadogo
ambao wengi wao wapo vyuoni na mashuleni.
Na Kwa
vile kulikuwa na maswali mengi niliyoulizwa nini cha kufanya kwa ambao tayari
wameshatoa mimba sasa ungana name ili tujuzane.
Mambo yenyewe ni haya…
ONANA NA MTAALAMU WA USHAURI:
Kama una mawazo mengi kwanini umetoa mimba na
unajutia maamuzi yako au moyoni unahisi umefanya kosa kubwa kwa binadamu au
mungu wako nenda unana na mshauri na atakusaidia kurudi katika hali yako ya
kawaida.
NENDA HOSPITALI UONANE NA DAKTARI;
Ukitoa mimba kuna madhara mengi yanayofuatia ikiwemo ugumba, na
kuharibika viungo vya uzazi.. nenda ukapige picha ya ultrasound
kuangalia hali ya viungo vya uzazi, na kama vinaumwa vianze kutibiwa mapema
iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika. Pia pima magonjwa mengine ya
kuambukizwa ikiwemo ukimwi, kaswende na gono kwani ni magonjwa yanayo
ambatana na ngono zembe. usiogope hakuna daktari wa kukupeleka polisi kwa kutoa
mimba..
CHAGUA NJIA YA UZAZI WA MPANGO:
Kuna watu wameshatoa mimba mpaka tano sasa hivi,
mimi naona huo ni uzembe kwani kuna njia nyingi sana za kuzuia ujauzito. Kama
huwezi kondomu njia ya kijiti ni nzuri kuliko zote kwani siku ukitaka mtoto
unakitoa kijiti na kunasa mimba haraka. njia ya kalenda ni nzuri pia ila wengi
hawaiwezi na inataka umakini sana hivyo achana nayo..Acha kusikiliza kelele za
watu eti njia hizo zina madhara kwani hizo ni imani potofu na ukipuuzia
utaendelea kutoa mimba zaidi kitu ambacho ni hatari kiafya.
TUMIA VIRUTUBISHO VYA
UZAZI;
Mara nyingi
kutoa mimba huharibu mfumo wa homoni za uzazi wa wanawake na maumbile ya
uzazi. Hali hii ni hatari na ndio
hufanya wanawake wengi kushindwa kubeba mimba siku za usoni. Tumia virutubisho vya multmaca ambavyo vimesaidia sana
kurudisha hali ya homoni katika kawaida yake na kusaidia kubeba mimba kwa
wanaozitafuta.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv