Kama  hujui kuitunza miguu yako basi ni kwamba  Mtu yoyote anaweza kupata hili tatizo. Inaweza kukutokea  kama hupaki moisturizer, ndio hata miguu yako nayo inahitaji moisturizer, ikikauka sana inaanza kuchanika na hata kuzua matatizo mengine.


Vitu vinavyosababisha ukavu mpaka kupasuka nyayo ni
1.Kutembea sana peku
2.ukali wa jua na miguu unaikanyaga chini
3.Kuogea sabuni ambazo hazina moinsture
4.tatizo la kisukari na thyroid
5.kuogea maji ya moto kupitiliza kila siku
6.matatizo ya ngozi eczema ambayo hupelekea ngozi kuwa kavuu

Unatibu vipi ukavu wa nyayo?
kuna watu ambao tayari wana asili ya ngozi kavu hivyo ni lazima wafanye kazi ya ziada kulainisha miguu.

1.Ukimaliza kuoga tu unahakikisha unapaka nyayo zako mafuta au lotion zenye moinsture.Usipake lotion zenye kemikali au alcohol huzidisha ukavu wa miguu.Paka hata mafuta ya watoto ambayo hayana kabisa kemikali.

2.Pia unaweza kuloweka miguu yako kwenye maji yenye juice ya limao,juice ya limao husaidia kuondoa zile dead skin
3.Paka miguu yako mchanganyiko wa kijiko kimoja cha olive oil na matone kadhaa ya limao.Changanya vyema kisha paka kwenye nyayo ili kuipa moinstrure yaani unyevu unyevu.

4.Unaweza kutengeneza scrub yenye mchanganyiko wa unga wa mchele,olive oil,veniger na asali.Unazifanyia scrub nyayo zako na huo mchanganyiko.

5.Ukishasafisha na kufuta miguu yako paka vegetable oil...mafuta kama hayo ya olive na mafuta natural kabisa ya nazi.
Haya ni mafuta ya nazi natengeneza MIMI mwenyewe kiasili kabisaa yatakufaa kwa miguu na nyayo zilizo kavu.Ukivutiwa na wewe huwezi kutengeneza mwenyewe tuwasiliane.Tayari nimewauzia wengi tu kwa ajili ya kupaka watoto wao na hata watu wazima wanaopenda mafuta ya nazi.
Ukiyapaka kabla hujaenda kulala vaa socks ndio ulale.Fanya hivi kila siku.

6.Kabla ya kulala Chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako.Fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka.Vaa socks zako ndio upande kitandani kulala.

kwa ufupi Unaweza kuponya miguu yako kwa kufuata njia ifuatayo

Kabla ya kulala chukua beseni, weka maji kisha chukua Listerine changanya kwenye maji. 

Loweka miguu yako kwa dakika 20. 

Toa, then paka moisturizer uliyonayo, wengine hutumia glycerine, sheer butter, olive oil na vingine.

Vaa socks za cotton na lala nazo



JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top