Mapaja ya ndani na makwapa hutokea weusi kutokana na
msuguano wa ngozi kwasababu ya mapaja kugusana, hata ngozi iliyokauka pia
inaleta weusi katika ngozi.
Hivyo nimekuletea njiaasili ya kuondoa
weusi huo bila kutumia madawa makali.
TUMIA
MAFUTA YA NAZI NA NDIMU.
Mafuta ya nazi yanatumika kulainisha ngozi
lakini unaweza kutumia pia katika kuondoa weusi ukichanyanya na ndimu..fuata hatua
hizi::
*Chukua vijiko 3 vya mafuta ya nazi changanya na ndimu
nusu
*Paka sehemu yenye weusi katika mapaja huku ukisugua kama
unafanya massage kwa dakika 15.
*Kisha
osha na maji ya uvuguvugu na kausha kwa kitambaa kilaini na kisafi.
TUMIA
MCHANGANYIKO WA SUKARI ASALI NA NDIMU.
Mchanganyiko huu pia unaweza ukaondoa weusi
katika mapaja na makwapa, fuata hatua hizi::
*Changanya kijiko kimoja cha asali, ndimu nusu na kijiko
kimoja cha sukari.
*Paka sehemu yenye weusi na sugua kawaida hadi sukari
ipotee.
*Acha
ikae kama dakika 10 kisha osha na maji ya uvuguvugu.
GANDA LA
CHUNGWA NA ASALI
Kama mnavyojua machungwa yana vitamin C, na
hivyo ukichukua ganda la chungwa pamoja na asali, mchanganyiko wake pia
unaondoa weusi. Fuata hatua hizi::
*Chukua ganda la chungwa na kijiko kimoja cha asali.
*Kamua hilo ganda maji yake yangie kwenye asali.
*Kausha nakusaga hilo ganda kisha poda yake ichanganye na
asali
*Paka mchanganyiko huo katika sehemu yenye weusi, kaa kwa
muda wa dakika 15
*Osha
na maji ya kawaida hadi kugandaganda kupotee.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv