Moja ya hasara ya mwanamke aliye hodari na kazi za nyumbani ni
viganja vya mikono kuwa vigumu au vikavu.Kama unafua na maji na sabuni,kuosha vyombo,kusafisha
nyumba,kubadili watoto nepi au diapers,kupika n.k . usishangae kuwa
na viganja vigumu au vikavu.
Toa wasiwasi hii ni aina
ya kufanya mikono yako iwe laini na ya kuvutia.
Baada ya kazi zako fanya haya Kunywa maji kwa wingi na
kisha tumia njia hizi zifuatazo;
· Chukua container
weka chumvi kiasi.
· Weka
olive oil ndani ya container.
· Weka
sabuni ya maji ya kuoshea mikono,tumia aina unayoipenda inaweza kuwa
anti-bacterial au yoyote ya maji.Ni vizuri kutumia sabuni ya maji
sababu hautaosheka vizuri mkono sababu maji na mafuta hayachanganyiki.
· Kausha
mikono yako vizuri,kisha weka mchanganyiko huo kwenye viganja vyako kisha sugua
pole pole ,kiasi cha ½ kijiko cha chai.Sugua ndani na nje ya viganja na ndani
ya vidole na kucha.
· Osha
kwa maji ya uvuguvugu .
· Kausha
mikono kwa kutumia taulo kavu.
· Pakaa
lotion ya mikono .
· AU
· Osha
mikono na maji ya uvuguvugu na sabuni kuondoa grease na bacteria.kisha kausha
na taulo kavu.
· Chukua
sukari vijiko viwili(2) vya chai na olive oil pia vijiko
viwili(2).
· Pakaa
mikononi kwa pamoja haraka .
· Sugua
mikono yote kwa pamoja ndani na nje kwa kutumia mchanganyiko huo.
· Osha na
maji ya uvuguvugu.
· Tumia
rose water pia nzuri .
· Kisha
pakaa lotion ya mkononi.
· Waweza
tumia pia sunflower oil na hata mafuta ya nazi pia mazuri.
Kumbuka
·
Usifanye mara moja ukategemea matokeo ya kudumu au milele.
·
Tumia baby oil au lotion kabla ya kulala.
·
Tumia lotion zinazotengenezewa na mimea zaidi.
·
Acha lotion kwa dakika kumi(10)kwenye viganja,ile layer ya juu
ya ngozi itanyonya lotion na italoki moisture ndani ya ngozi.Fanya hivi mara
mbili(2) kwa wiki.
·
Vaa gloves au plastic wakati unafanya kazi kama kuosha vyombo au
gardening.
·
Tumia Vaseline.
Kwa mikono mikavu zaidi unaweza kulala na gloves ukiwa umepakaa
lotion.
Usiache mikono kwenye maji baridi kwa muda mrefu,huondoa mafuta
na unyevu wa asili mikononi.
Kuwa muangalifu na aina ya lotion utayotumia kuepusha athari za
allergies.
Unaweza kuzicheki Hizi ni aina ya lotion unaweza tumia
kulainisha mikono : The body
hemp hand protector, Aron moisture therapy intensive hand cream, L’Occitane
shea Butter Hand Cream, Eurin Intensive Repair Extra Enriched Hand Crème, Ahava
Source Mineral Hand Cream, Jaqua Raspberry Butter cream Frosting Hand Crème.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv