Meno yako yanaweza kuwa ya njano kutokana na vyakula na vinywaji tunavyokunywa, na pia inategemea ni vipi unatunza afya yako ya meno, kama unapiga mswaki vizuri, unasafisha vizuri au vipi. Kama meno yako si ya rangi ile inayotakiwa chagua kati ya hizi njia 2 kutumia mara moja kila wiki itakusaidia.

Baking Soda na juice ya ndimu.
Baking soda ina sodium bicarbonate ambayo inasaidia kuondoa madoa na rangi ukichanganya na ile juice ya ndimu inasaidia kupunguza alkaline iliyopo kwenye ndimu.
Changanya juice ya ndimu pamoja na baking soda kupata paste nzito, futa meno kuondoa mate kisha chukua mswaki wako chota mchanganyiko then paka kwenye meno (usipige nayo mswaki kama unavyotumia dawa ya mswaki, paka tu!), iache kwa dakika 1 kisha  sukutua na maji. Fanya hivi mara moja kwa wiki.

Tumia mafuta ya nazi.
Tumia mafuta ya nazi kila asubuhi kusukutua kabla hujapiga mswaki. Weka kisi cha kutosha mdomoni then anza kusukutua, zungusha katika kila kona, fanya kama unavuta na kuyasukuma humo mdomoni lakini usiyameze. Fanya hivi kwa dakika 10-15.

Ukishamaliza hivyo sukutua then piga mswaki kama kawaida.


JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog na  youtube@edone tv
 
Top