Chumvi
inaweza kutumika kama kipodozi na
kukuacha ukiwa na ngozi nyororo na ya kuvutia.
Pamoja
na kutumiwa kama kiungo katika mapishi mbalimbali. chumvi ina
umuhimu wake katika suala zima la urembo.
Kumekuwepo
na sababu mbalimbali zinazopelekea warembo kupata matatizo ya ngozi. Kitendo
hicho huwafanya warembo husika kupoteza nuru ya ngozi zao na pia matumaini ya
kuonekana wenye kuvutia na kupendeza. Kuna Matatizo ya chunusi, ukavu katika
ngozi, mafuta usoni na hata mlundikano wa ngozi zilizokufa usoni ni miongoni
mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kupelekea kutumia vipodozi
visivyo salama kwa ngozi zao.
Kwa
kutambua hilo wataalamu wa urembo wa asili walikuja na njia hii ambayo haina
gharama kubwa ukilinganisha na njia zilizozoeleka na warembo wengi. Matumizi ya chumvi yamekuwa na
matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi, ingawaje si wengi
wanalolifahamu hili.
Unachotakiwa kuzingatia ni kuhakikisha kuwa chumvi hiyo haingii
machoni mara utakapoanza kuitumia.
Mahitaji.
Chumvi ya unga kijiko 1 kikubwaNamna ya kufanya
**Nawa uso wako kwa maji ya
kawaida na kisha chukua kitambaa laini na safi. Chovya kwenye chumvi na kisha
sugua katika ngozi yako ya uso taratibu.
**Baada ya kupaka katika uso
mzima, weka chini kitambaa chako na kisha jisugue kwa kutumia mikono yako.
Fanya hivyo hadi utakapoona takataka zinatoka.
**Baada ya kufanya hivyo kwa muda
wa dakika mbili, osha kwa kutumia maji ya baridi.
**Ni muhimu kufanya zoezi hili
mara kwa mara kwani bila hivyo krim au losheni yako unayotumia haitafika katika
ngozi pindi unapotaka kufanya hiyo.
**Unashauriwa
kufanya aina hii ya scrub mara moja kwa wiki ili kupata matokeo mazuri.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv