kuna baadhi ya wanawake ambao ni waongo sana, na hiyo
inajulikana, hata kuwashinda wanaume ambao inajulikana wao ndo wajanja katika
kudanganya kuliko wanawake,
lakini leo tutaangalie
vile vitu ambavyo wanawake wengi huwa wanadanganya sana.
1. Umri
Wanawake wengi
wanaamini wanaume wanavutiwa na wanawake wenye umri mdogo, wanawake walio na
miaka kati ya 24-29 mara nyingi huwa wanashusha miaka 2 hadi 3 ili waonekane
wadogo mbele ya wanaume.
2. Kutokuwa Na Mahusiano
Baadhi wa wanawake,
husema wapo kwenye mahusiano hata kama hawapo,hii inatokea hasa kama mwanamke
hamtaki mwanaume aliemtokea wakati huo na kisingizio kikubwa ni yeye kuwa
katika mahusiano na huu ni uongo mmoja maarufu sana na Baadhi ya wanawake pia
huwa wanaficha kama wapo kwenye mahusiano, hasa pale wanapotaka kuanzisha
,mahusiano mapya, huku wakiendelea kuwa na mahusiano na wanaume wawili kwa
wakati mmoja.
3. Mara ya mwisho kukutana kimwili na
mwanaume
Mwanamke hawezi
kukwambia ukweli kuhusu hili hata kama alikutana na mtu kimwili jana,
atakwambia miezi 4-8 iliyopita, hii ni kwasababu anaona ataonekana muhuni sana
au Malaya, na wengi wao huwa wanataka kuonekana wasafi au tuite watakatifu.
Kitu ambacho sio
4. Ameshakuwa na wapenzi wangapi
Uongo mwingine ambao
ni maarufu ni kuhusiana na mwanaume wangapi ametoka nao, hapa sahau sana kwani
huwezi kupata jibu sahii, sababu wanawake wengi huwa wanadanganya mahusiano yao
ya nyuma, anaweza kukwambia wawili au watatu kitu ambacho inaweza kuwa zaidi ya
hao. Japokuwa uongoo huu hata wanaume pia wanadanganya
5. Kudanganya kuhusu vitu alivyozoea
Wapo wanawake wanadanganya
kuhusu kutoka usiku, labda sio watu wa tungi/Gambe, sio watundu kitandani na
kujidai ndo kwanza kuna mambo wanayaanza siku hiyo. Kujidai hawawezi hiki mara
kile mara akwambie mie ndo mara yangu ya kwanza ilimladi vituko .
Ila mwanamke mpaka
anafikia stage ya kudanganya haya ni kwa sababu ana mapenzi ya dhati na mtu
huyo na anaogopa kumpoteza kama akijua baadhi ya vitu vyake vya ndani. Japokuwa
wakati mwingine hali hii haijengi bali inabomoa mahusiano.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv