Tukiangalia Katika
ulimwengu wa mapenzi kuna mambo kadha wa kadha yanayo weza kusababisha watu
wazima kuamua kuingia kwenye mahusiano na watu wenye umri mdogo.
Leo
edonetz tunaangazia sababu za watu wenye umri mkubwa kupenda kuwa kwenye
mahusiano na watu wenye umri mdogo na kinyume chake.
URAHISI
WA MAISHA –
Vijana
wengi wakileo wanapenda mteremko; mara nyingi hupenda maisha ya bwerere yaani
mteremko pasipo kujishughulisha. Mara nyingi hupenda vya bure na kuamua kuingia
kwenye mahusiano na mtu aliyemzidi umri kupita kiasi na hii inatokana na baadhi
yao kuwa katika hali ya ugumu wa maisha.
PESA
imekuwa
na ushawishi mkubwa katika suala zima la mahusiano. Mabinti wenye umri mdogo
wamejiingiza katika mahusiano wa wanaume wenye umri mkubwa sambamba na vijana
wakiume wenye umri mdogo kupenda kulelewa na wamama waliowazidi umri ili
kujipatia pesa.
KUEPUKA
USUMBUFU.
Hapa
mabinti wengi huamini njia pekee ya kuepuka msongo wa mawazo katika mahusiano
ni ‘kudate’ na wanaume wenye umri mkubwa kuliko wao kwa kuwa wanaamini
hawapepesi macho kama vijana wenye umri sawa na wao. Pia wanaamini wanaume
wenye umri mkubwa hawana wivu wala muda wa kuwa fuatilia nyendo zao kila mara.
UHITAJI
WA MTOTO
kwa
kuwa na hakika ya kuwalea kutokana na uwezo wa kipesa walionao. Vijana wa kiume
wa nyakati hizi huepuka kuzaa na mabinti kwa kuwa hawapendi majukumu, hupenda
starehe ndio maana hupendelea kulelewa.
KUFUATA
RAHA YA PENZI
ambayo
inadaiwa kuwa wanaikosa kutoka kwa waume zao halikadhalika Inasemekana wamama
hupenda vijana ambao damu inachemka ili kufurahia raha ya penzi.
MALUMBANO
NDANI YA NDOA YALIYO SUGU.
Magomvi
na kero zinazoibuka siku hadi siku husababisha mwanamke/mwanaume kutafuta
binti ama kijana mbichi atakaye mtuliza moyo na kumsahaulisha machungu anayo
yapata ndani ya ndoa.
JIUNGE NASI
KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na
youtube@edone tv