Karibu sana msomaji wa edonetz katika makala zetu za
kila siku kuusu maisha ya kila siku na leo tunaelekea kuzungumzia namna ya kuepuka maumivu katika mapenzi.
NB unatakiwa kulike page zetu katika fb,kutufollow twiter,inster kwa
jina la edonetz hii itakusaidia kupata story zote punde zitokapo..
Tuanze kama ifuatavyo
JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU:
Hakuna jambo ambalo hutuliza fikra
na hisia za mapenzi kama kukubali kumsamehe yule aliyekuudhi kabla
hata hajakuomba msamaha na kuamua kusahau yote yaliyotokea.
Yawezekana wengi mtasema haiwezekani.
Marafiki, lazima kila mmoja aelewe kwamba unapokasirika au
kuumizwa, anayeteseka siyo yule aliyekusababishia maumivu bali ni wewe
mwenyewe.
Hasira au maumivu ya
kimapenzi huwa kama moto mkali ambao huitafuna taratibu nafsi ya
mhusika. Ukisamehe maana yake unaupa moyo na akili yako nafasi ya
kupata sehemu ya kutulia na kuuzima moto ambao tayari ulishaanza kukolea
ndani yako.
BADILISHA MAZINGIRA/
MARAFIKI:
Baada ya kuumizwa na mwandani
wako, mbinu ya kubadilisha mazingira na marafiki husaidia sana kukupa
nguvu ya kukabiliana na msongo unaoweza kukusababishia madhara makubwa.
Unaweza kubadilisha
mazingira kwa kusafiri, kubadilisha mpangilio wa chumba chako cha kulala
na kuondoa vitu vyote vinavyoweza kukukumbusha hisia chungu za maumivu.
Taratibu utaona akili yako ikianza kusahau maumivu.
Yawezekana pia kuwa
mpenzi wako ulishamtambulisha kwa marafiki zako nao wakamuona kama sehemu
ya familia. Ukiendelea kujumuika na marafiki hao, watakuwa wanakukumbusha
hisia chungu zitakazoendelea kukutesa, jiweke karibu na marafiki wapya
wasiojua historia yako ya mapenzi, watakuwa sehemu ya faraja kwako.
JIPENDE, JITHAMINI:
Utafiti wa kisaikolojia umebaini kuwa baada
ya kutendwa kimapenzi, watu wengi hujishusha thamani na kudhani
huenda wana upungufu, kasoro au udhaifu fulani ndiyo maana wapenzi
wao wakawasaliti na kutoka kimapenzi na watu wengine. Kama ni
mwanamke, muda wote atashinda kwenye kioo akijikagua kama ana kasoro
kwenye sura na mwonekano wake. Mwanaume vivyo hivyo, atashinda akijiuliza
kuhusu uwezo wake wa kumfurahisha mwenza wake faragha au uwezo wake wa
kifedha. Kujipenda na kujithamini kuende sambamba na kuboresha mwonekano
wako, hakikisha muda wote unakuwa msafi na mazingira unayoishi pia
yanakuwa masafi.
SITISHA MAWASILIANO:
Unapokuwa na maumivu ndani ya moyo wako,
jambo la busara ni kukaa mbali na kusitisha mawasiliano ya aina yoyote na
yule aliyekusababishia maumivu hayo. Wengi hufikia hatua ya kubadili
namba zao za simu ili kupata muda wa kutafakari mustakabali wa uhusiano wao.
Kama alikuwa rafiki
yako kwenye Facebook au Twitter, ‘block’ mawasiliano naye, kama ni kwenye
simu sitisha kumtumia ujumbe mfupi au kumpigiapigia simu, iache akili yako
ndiyo iamue kama bado unahitaji kuendelea kuwa naye au la.
USITAFUTE WA KUZIBA
PENGO:
Kosa ambalo wengi hulifanya baada
ya kutendwa na wapenzi wao, ni kukurupuka na kuanzisha uhusiano
wa kimapenzi na watu wengine muda mfupi baada ya kuumizwa. Badala
ya kupunguza maumivu, utajikuta ukiongeza ‘stress’ kichwani kwani huyo unayedhani
atafaa kuziba pengo, anaweza kuwa na maovu kushinda hata huyo aliyekuumiza.
Jipe nafasi ya kukaa
mwenyewe na kufikiria maisha yako ya baadaye, amini kwamba maisha
yanawezekana hata ukiwa peke yako, kubaliana na kilichotokea na jiambie
kuwa hutaki kurudia makosa kwa kuanzisha uhusiano na mtu atakayeuchezea
moyo wako.
JIPE ZAWADI:
Huenda wengi wakashangaa kwamba inawezekanaje
kujipa zawadi mwenyewe? Inawezekana, tembelea duka linalouza zawadi
za kimapenzi kama maua, kadi nzuri, midoli au chocolate na
jichagulie unayoipenda zaidi. Jiambie kuwa hakuna anayekupenda zaidi ya
jinsi unavyojipenda mwenyewe, jipongeze kwani maumivu hayatajirudia tena.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv