Mambo mengi
yanayotokea kila siku katika maisha ya mapenzi, mambo hayo yana wezekana
kuwa ni ya lazima kutokea, unayasababisha mwenyewe au unaruhusu yatokee
bila ya sababu.
Kutokana na hayo yote, leo nitazungumzia baadhi ya wapenzi wenye
tabia za kutoa mambo yao ya faragha na kuyapeleka kwa mashoga au rafiki
zao.
Kila unachokifanya usiku, mchana au asubuhi na mpenzi wako, basi
mama au baba wa jirani anafahamu, mkikwaruzana kidogo, ukimnyima mwenzio haki
yake ya ndoa, basi mama au baba mwenye nyumba anajua kila
kitu kilichotokea.
Sidhani kama ni sawa, hili ni tatizo ni moja ya upungufu mkubwa
katika uhusiano, sasa utofauti wenu mkiwa mmevaa na mkiwa watupu uko
wapi ikiwa kila kitu unaenda kukianika kwa rafiki zako?
Unadhani yeye hapendi vitamu na vizuri au raha kama ambazo
umekuwa ukimsimulia? Unadhani yeye hapendi raha na ujuzi ndani ya sita
kwa sita!
Usitengeneza mazingira ya kumshawishi mtu dhidi ya mpenzi wako,
ya chumbani yabaki kuwa ya chumbani na ya sebuleni yawe ya sebuleni,
pia ya kijiweni au saluni yaishie huko huko. Usichanganye ya chumbani
na sebuleni au saluni kuwa sehemu moja, utakuwa umeharibu sana.
Kama kuna kosa kubwa ambalo ulikuwa hulijui linaweza kukumaliza
kwenye uhusiano basi ni mwanaume au mwanamke kuwasimulia rafiki zake
kuwa mumewe au mkewe anayaweza mambo fulani au ana upungufu fulani.
Kwanza inashangaza sana unawezaje kusimulia mambo nyeti kiasi
hicho, mambo ya faragha ni siri kama ilivyo usalama wa taifa, ndivyo
ambavyo unapaswa kuiona kuwa ni sekta nyeti sana.
Kwa kweli inasikitisha kuona kila unachofanyiwa na mpenzi wako unakwenda kuwaambia mashoga zako. Eti, ooooh! Jana bwana’angu kanifanyia hivi, kanigeuza hivi, kiukweli usiku wa jana nimeinjoy sana.
Kwa kweli inasikitisha kuona kila unachofanyiwa na mpenzi wako unakwenda kuwaambia mashoga zako. Eti, ooooh! Jana bwana’angu kanifanyia hivi, kanigeuza hivi, kiukweli usiku wa jana nimeinjoy sana.
Kwa penzi la mpenzi wangu, nashukuru Mungu nimempata mpenzi
anayeyajua mambo, kwa hilo sina shaka kabisa, Tabia hii ipo kwa pande
zote mbili, wanaume kuhadithiana na hata wanawake pia kufanya hivyo,
lakini siyo wote. Unakuta kijana yuko kijiweni na washikaji zake kakazana
kuwasimulia wenzake, Mwajuma ni mjuzi faragha, anajua kuzungusha nyonga
hakuna mfano wake, mwanangu yaani nashindwa namna ya kuelezea wewe elewa
mambo anayaweza.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv