Inashauriwa kwa mwanawake kusitisha kwa muda purukushani za huba
pindi atakapobaini kuwa mwenza wake anavuta kasi ya kuongeza gia.
Isitoshe dondoo za mazungumzo zinashauriwa sana kuchukua nafasi, isiwe ni
kasi kwa kwenda mbele kana kwamba mapenzi ni mchezo wa kukomoana au
ni pambano la kumpata mshindi. Mapenzi hayako hivyo na sio lazima
yafanyike kwa mhemko mkali kwa kipindi chote kana kwamba ni mbio za mita
mia.
Pamoja na hayo wanawake wanashauriwa kutoa angalizo la umbali
wao katika kufikia kilele ili kumpa fursa mwanaume naye kupata kipimo
cha wakati wa kumaliza. Angalizo hilo litamsaidia kumfanya apoteze
mawazo kwa hofu ya kuonekana hafai kwa kitendo cha kumwacha mwenzake
njia panda. Kusema kweli hili sio tatizo kubwa linalohitaji tiba ya
matatibu kwa kiasi hiki, isipokuwa ni kupata elimu ya kutambua uwezo wa
miili yetu.
Kwa maana hiyo maelezo ya dondoo zifuatazo yanaweza kumsaidia
mwenye tatizo hili.
UMRI WA
MTU:
Kuna baadhi ya wanaume wengine wa ajabu sana; wanajikuta
wakihangaika kutafuta dawa za nguvu za kiume eti kwa sababu hawaendi kama
zamani ilhali wanajua fika nguvu za mwili hupungua kutokana na
umri unavyokwenda.
MAZOEA YA
MWILI:
Watu
wengi wenye majukumu hujikuta wakiizoeza miili yao kwa kufanya mapenzi kwa
tendo moja kutokana na kukosa nafasi, kwao kukutana na mwanamke kwa maana
hiyo miili yao hukosa hamasa ya kurudia kutokana na mazoea. Hivyo muhusika
anapotaka kwenda raundi nne lazima aanze kuuzoeza mwili kidogo kidogo
asifikiri atakurupuka mara moja na kwenda mara tano.
HAMASA
KUSHUKA:
Upofu mwingine wa kimawazo ni kwa wanaume na
wanawake kutotambua kuwa hamasa ya kimapenzi hushuka kulingana na muda wa wapendanao
kuwa pamoja. Kuna wengine wanadhani kuwa watadumu kwenda mara sita au saba
kama walivyokuwa wakati wa uchanga wa penzi lao.
Katika hili wanapaswa kutambua siku zote mwili wa mwanadamu una
desturi ya kuzoea kile ambacho kinafanyika kila siku. Hivyo basi kabla ya kwenda hospitali au
kubwia madawa ya kuongeza nguvu jiulize maswali juu ya mazoea yako.
Na kama ukitaka kubadilisha mazoea hayo kumbuka kuwa haitakuwa
jambo la leo bali litachukua muda kuliwekea kumbukumbu katika mwili wako. Hivyo
basi nawashauri wale wote ambao wanashindwa kurudia kufanya tendo wafanye
utafiti juu ya nini kinapungua katika ushindwaji wao.
Lakini pia wasikubali kukata tamaa na kujiona hawawezi eti kwa
sababu wamekutana na mwanamke fulani na wameshindwa kufanya hivyo.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv