Ni wazi kwamba katika migogoro mingi ya mahusiano simu imekuwa
kichocheo kikubwa cha wapendanao au wanandoa kugombana. Simu ndizo
zinazoleta uhasama na kuvunja ndoa nyingi. Simu ndizo zinawafanya watu
wengi waliopo kwenye uhusiano kugombana.
Miaka ya nyuma, hususan wakati simu za mkononi zilipokuwa
hazijaingia nchini, matatizo kwa wanandoa au wapendanao yalikuwa machache
sana kulinganisha na sasa baada ya ujio wa simu.
Bahati mbaya sana, kati ya kesi nyingi za simu, zipo ambazo
zinakuwa na ukweli lakini nyingine huwa hazina ukweli. Mtu anaanzisha
ugomvi kwa sababu tu ujumbe wa kimahaba umeingia kwenye simu ya mke
au mumewe. Hahitaji kuhoji. Atamtukana, atampiga na atafanya kila
linalowezekana kuhakikisha anaondoa hasira zake kwa kile alichokiona.
Kumbe pengine angejipa nafasi ya kutafakari, akahoji, labda
hata wasingefikia hatua ya kugombana. Anaanzisha ugomvi kumbe
yule aliyetuma ujumbe huo, mwenzi wake wala hamjui.
KAMA WEWE NI MOJAWAPO FANYA FANYA HIVI.
Suala la kwanza unalopaswa kufanya kabla hujaingia kwenye
uhusiano, mchunguze vizuri mhusika. Hakikisha ni mtu mwenye moyo wa
kuridhika.
Tunaposema moyo wa kuridhika maana Awe tayari
ameshaamua kuwa ‘serious’ na mtu mmoja.
Macho yake si ya kutangatanga. Hababaishwi na kila mwanamke au mwanaume
amuonaye. Mtu wa aina hiyo hafai. Atakupotezea muda. Atakusababishia
ugomvi kila wakati mbele ya safari. Anzisha uhusiano na mtu aliyetosheka
na ujana.
UAMINIFU NI NGUZO KUU
Ukishafanikiwa kuwa na mtu mwenye sifa hizo, kinachofuata ni
suala la uaminifu. Jenga imani kwa mwenzako. Mfikirie katika fikra chanya
zaidi na si hasi. Muamini kwamba hawezi kukusaliti. Ukimuwazia
mwenzako katika mazuri ni rahisi hata kukabiliana na wazushi
watakaokuletea maneno ya uongo ili kukugombanisha na mwenzi wako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv