Wataalamu
wa afya husema ubongo wa binadamu hufanya kazi kwa msukumo wa hali ya hewa na
mazingira kwa ujumla, kwa mfano
kukiwa na hali ya mvua ubongo utatafakari jambo kulingana na hali ya hewa
ilivyo kupitia milango ya fahamu na kama ni jua kali vivyo hivyo ubongo
utafanya maamuzi kulingana na hali ya hewa ilivyo.
Inashauriwa
mara tu unapoamka jambo la kwanza unapaswa kujinyoosha viungo ili kuuweka mwili
sawa kwani mawazo chanya hupatikana katika hali ya hewa iliyotulia mathalani
kwenye miti mingi ambapo hewa safi hupatikana, kwenye milima na maporomoko ya
maji au maeneo yenye uoto wa asili.
Wanasaikolojia
wanautaja uoto wa asili kama njia bora ya kutibu mtu anayesumbuliwa na msongo
wa mawazo kwa kuikutanisha akili na uoto wa asili; mbali na njia ya kumfanyia ‘cancelling’, mtu huyu anapopata fursa
ya kukaa maeneo yaliyotulia na yenye hewa safi kwa kiasi kikubwa husaidia
kupunguza ama kuondoa kabisa msongo wa mawazo.
Mara
nyingi hushauriwa kutembelea maeneo ya mbuga za wanyama, kwenye milima, chemchem, mito, bahari,
maziwa na maeneo yaliyozungukwa na miti mingi.Msongamano uliopo
maeneo ya mijini unaosababishwa na uhaba wa ajira, huchangia msongo wa
mawazo kutokana na hali ya joto ambalo ni zao la moshi na mvuke kutoka
viwandani pia kelele za magari, wapiti njia pamoja na magari.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv