Wengi
wetu, tunatumia mikono kuosha uso…si ndiyo? Lakini unachotakiwa kujua ni kuwa
mikono yetu hata kama huwa una nawa kwanza bado inakuwa na bacteria kwenye
kucha na vidole.
Kwenye
urembo si salama sana kutumia mikono yako. Kwahiyo ni vizuri ukatumia kitambaa
maalumu kwaajili ya kujisafshia.Tafuta kitambaa kilaini na kisafi ndio uwe
unatumia kuoshea uso wako.
Osha
uso wako mara 2 kwa siku, kama unavyopiga mswaki mara 2 kwa siku. Asubuhi na
usiku kabla hujalala, hakikisha unatoa makeup yote vizuri. Hata kama haupaki
makeup osha uso wako kuondoa jasho, mafuta na vumbi.
Wakati
wakuosha uso wako usisahau hii sehemu ya juu yani eneo la komo.Usisahau
Wengi huwa hawaoshi vizuri uso sehemu ya paji
la uso wakiogopa kulowanisha nywele zao au kuharibu style waliyoiweka.
Unachotakiwa
kufanya ni kutafuta kofia ambayo utakuwa unavaa ili kuondoa nywele usoni na
hakikisha unaosha uso wako vizuri.
Ukipata
vitambaa vyakuoshea uso vile vinavyotumika kwaajili ya watoto ni vizuri zaidi
kwani vinakuwa na pamba. pia unaweza kutumia kusafishia uso wako, ila hakikisha
ni 100% cotton.
Kuna wale pia wanaotumia mabrush au yapo ya
aina nyingi kwahiyo unashauriwa kubadilisha brush zake angalau kila baada ya
mwezi au miez 2 na uchague brush laini. Chagua
sabuni itakayokufaa wewe kutokana na aina ya ngozi yako.
Tumia maji ya
uvuguvugu na usisugue. Baada
ya kuosha tumia taulo safi kukausha uso wako.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv