Kwanza razima ujue kuwa
kuna mtu maalum kapangwa kwa ajili yako, muda utafika tu na utapata furaha
unayoitafuta, usiogope kuanza upya kama ulipo hapakufai maana mapenzi
hayalazimishwi kwa namna yoyote ile.
Basi siku ya leo hebu
tuzione hizi sababu zinazokulazimu
umuache uliyenae katika mahusiano.
Kukuita
jina lisilo lako
Kila mara ukiwa nae
ndani na mnafanya mapenzi au anakubusu, anajisahau na kukuita jina lisilo lako,
huyo bado hajatulia na hajakuweka kwenye mipango yake bado, muache,
ukilazimisha sana utapotea.
Humuweki kwenye mipango yako
Upo nae lakini kila
mara unapowaza mipango yako ya baadae humuweki kwenye mipango yako na hata
unapokuwa naye mawazo yako muda mwingi yanakuwa mbali, huyo si chaguo lako,
muache uendelee na safari.
Mkali sana kwenye simu yako
Kila unapokuwa naye,
simu yake inakuwa yake na simu yako inakuwa yake pia, anasoma sms na kuwa mkali
sana kwenye simu yako ilhali yako wake huruhusiwi hata kuigusa, hakufai huyo.
Ugomvi nae kila siku
Kila unapokuwa na
ugomvi nae kila siku wewe ndio wa kumuomba msamaha hata kama yeye ndio
amekukosea, huyo hawezi kuwa na upendo wa kweli, mapenzi ni kusikilizana pande
zote mbili na si kwa upande mmoja kuonewa kwa kila kitu.
Anakupangia kila vazi
Kuvaa ni njia mojawapo
ya kujiamini kwa mwanamke, lakini inapotokea anakupangia kila vazi unalotakiwa
kuvaa na usilotakiwa kuvaa hapo inakuwa sio sawa, huwezi kutoka kwenda shule,
kazini, outing, na kwingineko mpaka aone ulichovaa.
Anakuchagulia marafiki
Anakuchagulia watu wa
kuwa nao ikiwa ni pamoja na marafiki, hii sio dalili nzuri, wanaume wanaotenda
‘madhambi’ pembeni ndo huwa na tabia hii kwa wingi, wewe unakuwa ni mtu wa
kubadili marafiki kila kukicha.
Mtu wa kukukopa pesa na kusahau
Linapokuja suala la
pesa mara nyingi huwa hakuna undugu, mara nyingi amekuwa ni mtu wa kukukopa
pesa lakini anajifanya kusahau inapokuja
muda wa kulipa deni, sio dalili nzuri ya mwanaume anayekufaa, una mipango yako
binafsi ukiachilia mbali mapenzi na yeyote atakayesababisha mipango yako
kutosogea mbele hatakiwi kuvumiliwa.
Anakuhitaji kwa ajili ya Kutimiza haja zake za
ngono
Mapenzi yake kwako
huongezeka pale tu anapokuhitaji kwa ajili ya kutimiza haja zake za ngono na
anapomaliza hukusahau na kukupotezea, hakufai kabisa huyo mtu.
Anakudharau
Kila unachomwambia
hukusikiliza na kukubaliana nawe lakini inapokuja wakati wa kutekeleza kwa
vitendo mlichokubaliana mambo huwa tofauti, ANAKUDHARAU na anajisemea
moyoni Bora Liende, hakufai huyo.
Anaona kazi zote ni za wanawake tu
Hawezi kila kitu cha
jikoni, hawezi kuosha vyombo hata kikombe cha chai, hawezi kupika hata chai,
hawezi hata kufua nguo zake za ndani na anaona kama kazi hizo zote ni za
wanawake tu, umejaribu sana kumuelekeza na haonyeshi mabadiliko, Kimbia.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv