Uwezo wa kutengeneza vipande vya mawe
vyenye makali na kuvitumia kazini uliwawezesha binadamu wa kale kuishi vizuri
duniani. Lakini hivi karibuni wanasayansi waligundua kuwa si binadamu tu wenye
uwezo wa kutengeneza vipande hivi.
Kima aina ya sapajus libidinosus wanaoishi huko Amerika ana uwezo
mkubwa wa kutumia mawe. Wanajua kuvunja kokwa kwa mawe na kuwavutia jike kwa
kuwatupia mawe. Dk. Tomos Proffitt wa Chuo Kikuu cha Oxford na wenzake walipotafiti kima hao katika
Bustani ya Taifa ya Serra da Capivara nchini Brazil, waliona kima hao wanaweza
kutengeneza vipande vya mawe ambavyo vinafanana na vile vilivyotengenezwa na
binadamu wa kale.
Kima hao wanapenda kugonga jiwe moja kwa jiwe lingine mara kwa mara na mara nyingi wanafanikiwa kutengeneza vipande vya mawe. Ingawa vipande vya mawe vyenye makali ni vifaa vizuri vya kukatia, lakini kima bado hawajui namna ya kutumia vipande hivi. Watafiti hawajathibitisha lengo la vitendo vya kima hao, lakini wameona kuwa baada ya kugonga mawe, kima hao huyalamba. Dk. Proffitt anafikiri huenda kima hao wanakula unga wa mawe ili kupata lishe ya silicon au wanakula kuvu kwenye mawe.
Lakini sasa watu wakigundua mabaki ya
vipande vya mawe yenye historia ndefu, hawawezi tena kusema moja kwa moja kama
vilitengenezwa na binadamu wa kale, wanahitaji kufikiria uwezekano kwamba
huenda vilitengenezwa na kima.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv